WAZIRI BALOZI DKT CHANA ARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA MSOMERA

 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana amefika Kijiji Cha Msomera wilaya ya Handeni mkoa wa Tanga kukagua hatua za maandalizi ya kuwapokea Wafugaji walioamua kuhama kwa hiyari yao ili kupisha shughuli za uhifadhi katika Hifadhi ya Ngorongoro.


Akizungumza na wakazi wa Kijiji hicho, Waziri Balozi Chana ameridhishwa na maandalizi yaliyofikiwa na kuupongeza uongozi wa Mkoa wa Tanga kwa usimamizi mzuri wa kazi na maandalizi hayo pamoja na wananchi wa Kijiji hicho kwa kishirikiana vyema na Serikali inayo ongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya maboresho makubwa Kijijini hapo.

Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa Msomera, Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mzee Martin Oleakae ameishukuru Serikali kwa kukichagua Kijiji hicho ili wafugaji kutoka Hifadhi ya Ngorogoro wahamie kwani maboresho ya huduma za kijamii yanayofanyika sasa yatawanufaisha wafugaji wanao hamia pamoja na wananchi wengine wa Msomera.







Post a Comment

Previous Post Next Post