NAIBU WAZIRI MASANJA ASHIRIKI MKUTANO WA WAZIRI WA MAMBO YA NJE, MABALOZI NA WAKUU WA MASHIRIKA YA KIMATAIFA

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amemuwakilisha Waziri wa Maliasili na Utalii katika Mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini kuwaelezea mpango wa Serikali katika kulinda na kuhifadhi eneo la Ngorongoro uliofanyika leo Juni 21,2022 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema kuwa Serikali imechukua jukumu la kukata eneo la Loliondo SQM 4000 ambazo zina usajili na eneo la SQM 2500 likakatwa kwa ajili ya matumizi ya Wananchi. 

Masanja amesema kuwa vyombo vya Habari vimekuwa vikipotosha kuhusu eneo hilo kwa kutaka kuharibu taswira ya wawekezaji nchini Jambo ambalo halina manufaa kwa Taifa.

" Vyombo vya Habari vinapotosha kuhusu mwekezaji aliyepo zaidi ya miaka 30 ambapo kila mwaka vitalu vya eneo Hilo hutangazwa kisheria na kuingizwa katika minada ambapo mwekezaji huyo huibuka mahindi na kupata eneo lake kisheria", alisema Masanja





Post a Comment

Previous Post Next Post