TTB YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA TAIFA VIJANA YA MPIRA WA KIKAPU

 Na Humphrey Shao, Michuzi Tv


Wizara ya Maliasili na utalii kupitia bodi ya Utalii Tanzania(TTB) imekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu ya Taifa ya vijana ya mpira wa kikapu inayoshiriki mashindano ya kimataifa nchini Uganda.

Akizungumza kwa niaba ya katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Tanzania,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB , Felix John amesema ufadhili huo una lengo la kutangaza utalii wa Tanzania kupitia michuano ya kufuzu fainali za afrika kwa vijana chini ya miaka 18.

"TTB inajukumu la kutangaza utalii hivyo leo tumetoa vifaa vyenye thamani ya shilingi 6,766,120.00 ambavyo ni pisi 24 za jezi za mpira wa kikapu rangi ya Blue , Pisi 24 za jezi za mpira wa kikapu tangi nyeusi , Pisi 35 za Traki suti juu na chini na pisi 48 za soksi" Amesema John

Umesema lengo ni kuwawezesha kushiriki ipasavyo na kushinda mashindano ikiwa na lengo la kuendeleza programu maalum ya Royal Tour ambayo imeasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Rais wa TBF Ndugu Michael Kadebe ameishukuru Wizara ya Maliasili kwa kuweza kusaidia na kuendeleza michezo nchini .

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB , Felix John akikabidhi moja ya jezi za mchezo wa kikapu kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu nchini Michale Kadebe


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB , Felix John, akikabidhi Traki suti kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu nchini Michale Kadebe 


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB , Felix John Akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo kwa timu ya Tiafa ya Vijana ya mpira wa kikapu inayokwenda kushiriki mashindano ya Zone 5 Uganda

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB , Felix John, akikabidhi mpira wa kikapu kwa Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu nchini TBF, Michael Kadebe 

Post a Comment

Previous Post Next Post