WIZARA YA MAJI YASAINI MKATABA WA BILIONI 1.4 KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA UPOTEVU WA MAJI KATIKA MANISPAA YA MUSOMA

 


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA), Mhandisi Nicas Mugisha na Meneja Biashara wa Kampuni ya CityTaps, Aurelie Guibert mara baada ya kusaini mkataba wa Shilingi bilioni 1.4 wenye lengo la kukabiliana na changamoto ya upotevu wa maji katika eneo la Mwisenge lililopo Manispaa ya Musoma, mkoani Mara.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akishuhudia utiaji saini wa mkataba kati ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA), Mhandisi Nicas Mugisha na Meneja Biashara wa Kampuni ya CityTaps, Aurelie Guibert wenye thamani ya Shilingi bilioni 1.4 wenye lengo la kukabiliana na changamoto ya upotevu wa maji katika eneo la Mwisenge lililopo Manispaa ya Musoma, mkoani Mara. Aliyesimama nyuma ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Wizara ya Maji, Simon Nkanyemka.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA), Mhandisi Nicas Mugisha (kulia) na Meneja Biashara wa Kampuni ya CityTaps, Aurelie Guibert mara baada ya kusaini mkataba wa Shilingi bilioni 1.4 wenye lengo la kukabiliana na changamoto ya upotevu wa maji katika eneo la Mwisenge lililopo Manispaa ya Musoma, mkoani Mara wakisaini mkataba wa thamani ya Sh. bilioni 1.4 wenye lengo la kukabiliana na changamoto ya upotevu wa maji katika eneo la Mwisenge lililopo Manispaa ya Musoma, mkoani Mara.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Equiplus, James Genga (wa kwanza kushoto) Meneja Biashara wa Kampuni ya CityTaps, Aurelie Guibert, Aurelie Guibert (katikati) na Afisa Uchumi kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Mashaka Ntobela katika hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa thamani ya Sh. bilioni 1.4 kati ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) na Kampuni ya CityTaps ya Ufaransa wenye lengo la kukabiliana na changamoto ya upotevu wa maji katika eneo la Mwisenge lililopo Manispaa ya Musoma, mkoani Mara.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza katika hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa thamani ya Sh. bilioni 1.4 kati ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) na Kampuni ya CityTaps ya Ufaransa wenye lengo la kukabiliana na changamoto ya upotevu wa maji katika eneo la Mwisenge lililopo Manispaa ya Musoma, mkoani Mara.

……………………………………………

Wizara ya Maji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) imeingia mkataba wa thamani ya Shilingi bilioni 1.4 na Kampuni ya CityTaps ya Ufaransa wenye lengo la kukabiliana na changamoto ya upotevu wa maji katika eneo la Mwisenge lililopo Manispaa ya Musoma, mkoani Mara.

Akishuhudia utiaji saini wa mkataba huo, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Sanga amesema mkataba huo ni muendelezo wa hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Wizara ya Maji kukabiliana na changamoto kubwa ya upotevu wa maji mijini na vijijini.

Mhandisi Sanga amesema kuwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) na Kampuni ya CityTaps ya Ufaransa waliandaa andiko la juu mkakati wa kupunguza kiwango cha upotevu wa maji kwa kutumia teknolojia mpya ya “Smart Meters” inayotumia mawimbi ya satelaiti kubaini mivujo ya maji ardhini lililopata kibali wizarani na kufanikiwa kupata ufadhili wa kiasi cha Shilingi 1,425,000,000 kutoka kwa Serikali ya Ufaransa. 

“Lengo letu ni kukabiliana changamoto ya upotevu wa maji mijini na vijijini ili kiwango kikubwa cha maji yanayozalishwa kiwafikie wanufaika pamoja na kuwezesha mamlaka kupata makusanyo ya kutosha yatakayowawezesha kuboresha huduma na shughuli zake za uendeshaji”, Mhandisi Sanga amefafanua.

“Natarajia ufanisi na matokeo mazuri katika utekelezaji wa mradi huu, ambao utadhibiti kiwango cha upotevu wa maji lakini pia kubaini sababu zinazosababisha upotevu wa maji na kuja mkakati bora wa kukabiliana na changamoto hiyo katika maeneo mengine nchi nzima”, amesisitiza Mhandisi Sanga.

Aidha, Katibu Mkuu Sanga ametoa shukrani kwa Serikali ya Ufaransa kwa ushirikiano inayoutoa kwa Serikali ya Tanzania hususani kwenye Sekta ya Maji na kusema kuwa pamoja na mradi huo, Serikali ya Ufaransa imefadhili miradi mbalimbali katika mikoa ya Dar es Salaam, Kagera na Morogoro.

Katika hatua nyingine, Meneja Biashara wa Kampuni ya CityTaps, Aurelie Guibert amemuhakikishia Katibu Mkuu Wizara ya Maji ufanisi katika utekelezaji wa mradi na kuja na mkakati bora utakaokua suluhisho la upotevu wa maji nchini Tanzania.

Mkataba huo umesainiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA), Mhandisi Nicas Mugisha na Meneja Biashara wa Kampuni ya CityTaps, Aurelie Guibert ni wa majaribio  na wa kwanza wa aina yake hapa Tanzania ambao utatekelezwa kwa muda wa miaka miwili. Pindi utakapokamilika na kufanikiwa utatekelezwa kwenye Mamlaka za Maji za nchi nzima.

Post a Comment

Previous Post Next Post