WAZIRI MCHENGERWA AITAKA SERENGETI GIRLS KUMPA HESHIMA MAMA SAMIA

Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema watanzania   wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan wanaitaka timu ya Taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Girls) kuleta ushindi wa heshima katika mechi ya marudiano dhidi ya timu ya Cameroon   ya kufuzu mashindano ya soka ya dunia kwa kuibamiza mabao mengi kuliko ushindi wa mabao manne kwa nunge uliopatikana  kwenye mechi ya awali Mei 22, 2022 nchini Cameroon. 

Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo alipoitembelea timu hiyo akiambata na Naibu Waziri, Mhe. Pauline Gekul, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi wa Michezo nchini pamoja na Viongozi  Wakuu wa Shirikisho la soka Tanzania na Zanzibar kwenye uwanja wa Amani uliopo Zanzibar ambapo amefafanua  kuwa watanzania wanaimani kubwa na timu hiyo ili kuandika historia  ya  kuwa timu ya kwanza Tanzania kufungua  milango ya Tanzania kuingia mashindano ya dunia mwaka huu.

“Na msikubali kufungwa hata goli moja kwenye mechi hii na huo ndiyo ushindi wa heshima, na heshima hii mtaipeleka kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar. Mhe, Dkt. Hussein Mwinyi na watanzania wote kwa ujumla” amesisitiza  Mhe. Waziri Mchengerwa

Amesema ndoto ya Rais Samia ni kuona kuwa timu hiyo inapiga hatua kwenye mchezo huo ili kulipeleka taifa la Tanzania kwenye mashindano ya dunia na amewaomba kuweka uzalendo na utaifa mbele.

Aidha, amesema Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anapambana kujenga  miundombinu  na viwanja vya michezo na amefafanua kwamba  hata kama Serikali ikiwekeza kwa kiwango gani kwenye sekta ya michezo lakini endapo  wachezaji wasipokuwa na nidhamu, kuzingatia maadili na uzalendo na utaifa haitasaidia kupiga hatua kwenye  michezo.


"Nataka niwaambiae hitoria ya Tanzania katika soka inaanzia kwenu, tumekuwa tukishiriki mashindano mbalimbali mara kadhaa lakini hatufiki popote, naamini hata ninyi mnajua hili!.  Ni kwa sababu hii nadiriki kusema Mwenyezi Mungu ameamua ninyi muanzishe historia soka  duniani katika nchi yetu,  kwa hiyo jukumu mlilonalo  ninyi  sasa ni kuhakikisha kuwa matamanio na ndoto za watanzania ambazo wamekuwa wakiziota  miaka mingi za kushiri kwenye  mashindano ya dunia kwenye soka mnayatimiza, na kamwe msibweteke kuwa kwa sababu mliwafunga Cameroon  mabao manne kwao”amefafanua  Mhe. Mchengerwa

Amesema vipaji hiyo walivyonavyo kama wataweza kuyabeba na matumaini ya watanzania walio wengi wenye hamu ya kujua kitachoitokea katika mchezo ujao basi mtaji wao ni vipaji vyao wao kwa maana ya kuwa  vipaji vyao ndiyo mtaji wao wa kufungua na kuboresha maisha yao. 

Amesema watanzania wengi wamekuwa na hofu kuwa Tanzania haiwezi kupiga hatua kwenye soka pengine kwa sababu hakuna miundombinu ambapo amesema  hiyo siyo kweli kwa kuwa  timu hiyo imefika kwenye hatua hiyo ya juu kabisa kwa  kutumia miundombinu hiyohiyo.

Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo, Nohela Luhala amemthibitishia Mhe. Waziri na ujumbe wake  kuwa watapambana kufa na kupona ili kuhakikisha kuwa wanaingia kwenye mashindano hayo ambayo yatafanyika nchini India  mwaka huu. 

“Ninaomba kukuhakishia Mhe. Waziri kuwa kama Mhe. Mama yetu kipenzi na Rais wetu Samia Suluhu Hassan alivyokuwa Rais Mwanamke wa kwanza kuiongoza Tanzania na sisi itakuwa timu ya kwanza nchini kuiingiza Tanzania kwenye mashindano ya dunia ya soka” amesisitia Luhala.   

Naye Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Pauline Gekul amewapongeza wachezaji   hao na kuwataka kuendelea kuwasikiliza walimu wao ili kufika  mbali zaidi kwenye mashindano ya kimataifa.

Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi amesisitiza kuendelea kufanya jitihada  zaidi  kweny mchezo unaofuata huku wakimtegemea  mwenyezi mungu kwa kuwa na Subira na haki kama maandiko kutoka kwenye  vitabu  vitakatifu  vya Qurani na Biblia ambapo mkurugenzi wa Michezo nchini Yusufu Omary Singo amesema  timu hiyo imekuwa na nidhamu kubwa ukilinganisha na timu nyingine za soka na kwamba imechaguliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye michezo ya Olympik  nchini Ufaransa. 

Rais wa Shirikisho la soka Zanzibar Abdiratifu Ali Yasin ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa mahusiano mazuri ya kuunganisha mashirikisho, vyama vya michezo na Serikali kwenye michezo.

Katika ziara hiyo Mhe. Mchengerwa na ujumbe wake walikula chakula cha pamoja na timu hiyo



 

Post a Comment

Previous Post Next Post