COSTECH YAJIVUNIA MAONI YA WADAU YENYE LENGO LA KUBORESHA, YATAKA BUNIFU ZINAZONUNULIKA

 Na Said Mwishehe, Michuzi TV


SERIKALI kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imesema wanajivunia kupata mrejesho wa wadau ubunifu nchini ili kuwa na ubunifu zenye tija huku ikitoa rai kwa wabunifu kuhakikisha wanabuni bidhaa zitakubalika kwa mlaji.

Akizungumza  Mei 12, 2022 jijini Dar es Salaam ambako kumekuwa na Wiki ya Ubunifu Tanzania kwa kuwakutanisha wadau mbalalimbali, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dk.Amos Nungu amesema pamoja na mambo mengine ni vema kuwa ubunuifu zenye kuleta maendeleo.

“Kupitia Wiki ya Ubinifu ambayo imefanyika kwa siku tatu hapa Dar es Salaam tunachofurahi ni kuona ushiriki mkubwa wa wadau sambamba na kupokea maoni na mawazo yenye lengo la kuboresha bunifu zinazobuniwa na Watanzaniana.Kupitia maoni ya wadau tutajua tuboreshe wapi

“Maana kazi ya Serikali jukumu lake kubwa ni kuweka mazingira wezeshi , sera, miongozo na miundombinu.Kupitia jukwaa hili la wiki ya ubunifu tumeshuhudia wabunifu wakionesha bunifu zao, wametoa mawazo na maoni yao na serikali inapokea,”amesema.

Aidha amesema kuwa na Wiki ya Ubunifu kitaifa ndio mara ya kwanza lakini huko nyuma imeshafanyika mara nane huku akifafanua mwaka jana wakati wa Wiki ya Ubunifu Waziri Mkuu alikuwa mgeni rasmi na akaagiza wiki hiyo kufanyika katika Wilaya na Mikoa yote nchini.

Amesema mwaka huu wameanza na mikoa 15 na cha kujivunia sehemu kubwa ya wiki hiyo zimeshikiliwa na kumbi za bunifu ambazo zinatoka serikalini na sekta binafsi.

“Wiki ijayo kuna nini Dodoma, jibu ni kwamba tutakuwa na kilele cha Wiki ya Ubunifu na katika wiki hiyo tutawatambua washindi wa mashindano ya sayansi na teknolojia.Tulifungua dirisha mwaka 2021 wabunifu waliomba na kisha wakachuja.

“Hivyo wiki ijayo wale ambao watatambuliwa wataitwa COSTECH ili kuona namna ya kuwaendeleza.Jambo la kufurahisha wameendelea kujitokeza wadau wengi katika eneo la ubunifu na wamekuwa wakisaidia katika sekta mbalimbali.

“Kwa hiyo wabunifu huko mbele watapata usaidizi wa moja kwa moja.Hata hivyo kwenye hizi bunifu ambazo vijana wetu wanakubuni ziko bunifu nzuri ambazo ni nzuri kuonekana kwenye maonesho lakini mlaji wa mwisho hayuko tayari kuilipia,”amesema.

Dk.Nungu amesema kwa hiyo katika kilele cha Wiki ya Ubunifu Dodoma kutakuwa na mafunzo kwa wabunifu wote ambao walishiriki kwenye shindano la sayansi na teknolojia ili watambue namna ya kuwa na bunifu ambazo zitakubaliwa na walaji.

“Kuna bunifu nyingine kweli vijana wetu ni watundu wanaangalia kwenye vitabu, wanaangalia huko duniani halafu wanatengeneza lakini ni kwa mazingira ya huko sio mazigira ya Tanzania, kwa hiyo ili ubunifu uwe wa tija ni mlaji kuweza kununua ,”amesema Dk.Nungu.

Kwa upande wake Mkuruegenzi Kidijtali na Huduma za Ziada wa Kampuni ya Simu Vodacom Tanzania amesema Vodacom ndio wadhamini wakuu wa Wiki ya Ubunifu ambayo inakwenda na kauli mbio inayosema Ubunifu kwa maendeleo endeleo.

“Hivyo kwanini Vodacom iko mbele kabisa katika masuala ya ubunifu ni ukweli usioficha sisi DNA yetu iko katika ubunifu , ubunifu kwenye huduma zetu, ubunifu kwenye maeneo mbalimbali yanayoendana na tabia yetu na kauli mbiu yetu , tutaendelea kuongoza katika ulimwengu wa kidigitali yanayoleta matokeo chanya kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla.

“Leo katika majadiliano tulikuwa tunaongelea mageuzi katika bunifu kwa kujiuliza tulikotoka, tuliko na tunakokwenda .Kwetu Vodacom siku zote tumekuwa mbele katika kuleta huduma ambazo zimebuniwa kwa ubora zaidi katika huduma za kifedha, huduma za kupiga simu, katika michezo , hivyo tumekuwa mbele kuleta huduma ambazo zimebuniwa katika kuleta maendeleo endelevu.”

Wiki ya Ubunifu Tanzania imeratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na COSTECH pamoja na UNDP kupitia program ya Funguo na mdhamini mkuu wa wiki hiyo ni Kampuni ya Simu ya Vodacom.







Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) Dk.Amosi Nungu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa midahalo na majadiliano yaliyohusu nafasi ya bunifu katika maendeleo endelevu ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza Wiki ya Ubunifu Tanzania kilele chake kinatarajia kufanyika jijini Dodoma.Wiki hiyo imeandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na COSTECH pamoja na UNDP kupitia program ya Funguo wakati mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Simu ya Vodacom.


Mkuruegenzi Kidijtali na Huduma za Ziada wa Kampuni ya Simu Vodacom Tanzania Nguvu Kamando akifafanua jambo kuhusu udhamini ambao wameufanya katika Wiki ya Ubunifu na kwamba kampuni yao imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia kuendeleza sekta ya ubunifu .


Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose (wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa kongamano la Wiki ya ubunifu (Innovation week 2022) leo lenye mada ya ubunifu kwa maendeleo endelevu ambapo alizungumzia hali halisi ya ubunifu na teknolojia nchini na mategemeo yake kwa nyakati zijazo. Wengine katika picha hiyo ni watoa mada kwenye kongamano hilo kutoka taasisi mbalimbali.


Rosemary Mwakitwange (kulia) kutoka Taasisi ya East Africa Business and Media Training akielezea jambo wakati wa kongamano hilo.


Baadhi ya washiriki waliohudhuria majadiliano ya Wiki ya Ubunifu jijini Dar es Salaam wakiwa makini kufuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kongamano hilo.




Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) Dk.Amosi Nungu akisitiza jambo wakati wa kongamano hilo la Wiki ya Ubunifu Tanzania.


Sehemu ya vijana wa kitanzania ambao ambao wamebuni katuni za aina mbalimbali ambazo zinaweza kutumika kutoa elimu mbalimbali kwa jamii ya Watanzania wakionesha ubunifu wao wakati wa maonesho ya Wiki ya Ubunifu Tanzania.


Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye Wiki ya Ubunifu Tanzania ambapo wamepata fursa ya kushiriki kwenye kingamano ambalo lilikuwa linajadili nafasi ya ubunifu katika maendeleo endelevu.

Rosemary Mwakitwange kutoka Taasisi ya East Africa Business and Media Training akifafanua jambo kwa washiriki waliohudhuria Wiki ya Ubunifu Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post