*******************
NA FARIDA SAID, MOROGORO.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kujipanga kupokea watalii wataofika nchini kufuatia kuzindua kwa Filamu ya Royal Tour nchini Marekani na Jijini Arusha na Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan
Waziri Dkt Pindi Chana ametoa kauli hiyo mkoani Morogoro wakati alipofanya ziara kwenye ofisi za TAWA kwa lengo la kufanya ukaguzi na kujionea maendeleo ya kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo ili kuweka maandalizi manzuri kwa wageni wataokuja nchini kwa ajili ya utalii.
Pia ameipongeza Mamlaka hiyo kwa kutenga maeneo ya uwekezaji katika mapori ya akiba na maeneo mengine inayoimiliki ili kuendelea kuwavutia watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani huku akisema uwekezaji huo mkubwa uliofanywa na TAWA utaleta matunda hivi karibuni kufuatia Royal Tour
Alisema Tanzania imesheheni vivutio vingi zikiwemo Hifadhi,Fukwe,mapori ya akiba,mapori yanayomilikiwa na vijiji hivyo kupitia Filamu ya Royal Tour inaonyesha Tanzania kuwa ni sehemu nzuri ya kufanya utalii pamoja na uwekezaji.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Semfuko amemshukuru Waziri Dkt Chana kwa kufanya ziara katika Taasisi hiyo kwani itasaidia kuwajenga zaidi.
Kwa upande wake Kaimu Kamishina wa Uhifadhi wa Wanyamapori Nchini Bwana Mabula Misungwi Nyanda alisema Mamlaka hiyo imeweka mikakati ya kuwahudumia watalii wa ndani na nje ya nchi watakaofika katika maeneo yao.
Aidha amesema TAWA imejipanga kupokea watalii mbalimbali kutoka sehemu tofauti duniani wanafika kutembelea vivutia vinavyosimamiwa na Mamlaka hiyo yakiwemo mapori ya akiba ya Pande,Mpanga kipengere, Mkungunero, Kijershi, Swangaswanga pamoja na eneo la urithi wa Dunia la Kilwa Kisiwani na Songo Mnara ambayo yamekuwa yakiwavutia watalii wengi duniani.