TBS KUPOKEA CHETI CHA UMAHIRI

  Kaimu Meneja wa Kitengo cha Usimamizi wa Mifumo ya Ubora (TBS) Bi.Magdalena Sedemaki akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za TBS Jijini Dar es Salaam.

***********************

Shirika la viwango nchini Tanzania (TBS), linatarajiwa kupatiwa cheti cha umahili kutoka kampuni ya sadicas May 12,2022 jijini Dodoma kutokana na kukidhi vigezo vya kimataifa.

Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Usimamizi wa Mifumo ya Ubora (TBS) Bi.Magdalena Sedemaki amesema kuwa utolewaji wa cheti hicho ni uthibitisho wa utoaji wa huduma bora na kuifanya kampuni hiyo kuwapatia cheti hicho ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Uwezeshaji, Viwanda na Biashara huku wadau, wateja na mashirika mbalimbali wakitarajia kuwepo

Aidha utolewaji wa cheti hicho ni uthibitisho kuwa TBS inatoa huduma kwa mifumo ya kimataifa na kukidhi matakwa ya nchi mbalimbali.

Amesema kuwa cheti cha ubora wanachotoa TBS kimesaidia taasisi mbalimbali kupata masoko mengi nje ya nchi.

Akizungumza juu ya viwango vya usimamizi wa mifumo ya ISO, Meneja wa Metrojia Bi.Stella Mrosso amesema kubwa husaidia taasisi za umma na mashirika binafsi kuboresha utendaji kwa kubainisha michakato kufuatwa na kutekelezwa na taasisi hizo ili kufuata malengo yao.

Post a Comment

Previous Post Next Post