MKURUGENZI MNDOLWA AWAASA WATUMISHI TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO

 Serikali ina matarajio makubwa ya utekelezaji wa Miradi ya Kilimo cha Umwagiliaji kutokana na ongezeko kubwa la Bajeti ya fedha za miradi ya Maendeleo kwa Mwaka wa fedha 2022 – 2023, hatua hii ya Serikali ina lenga kuongeza uzalishaji wa Mazao ya chakula na Biashara kutokana na kilimo cha Umwagiliaji.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Reymond Mndolwa  alipokuwa akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Makao Makuu jijini Dodoma.

Kufuatia hatua hiyo ya Serikali kuongeza kiasi hicho cha fedha Shillingi Bilioni 146.5 Katika Sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji Bw. Mndolwa ametumia fursa hiyo kuwaasa watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kupendana kushirikiana, kufanyakazi kwa pamoja (time work) kwa kuzingatia weledi katika maeneo yao ya kazi.

Amesisitiza kuwa suala la kupendana na kuheshimiana katika Utumishi linaongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuleta amani.

“Tuheshimu kila mmoja aliyepo hapa, wote thamani yetu ni moja kwa sababu wote tunaitumikia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.” Alisisitiza

Bw. Mndolwa ameongeza kwa kusema kuwa watumishi wanao wajibu wa kuhakikisha wanatunza mali zote za Tume akitolea mfano magari na Mitambo inayotumika katika shughuli za ujenzi wa miradi ya Umwagiliaji.

“Nataka kila mtu ahakikishe anatunza mali ile aliyokuwa nayo” ili iweze kutusaidia kwa muda mrefu zaidi, itunze ione ni mali yako wewe, usione ni mali ya umma au serikali, sababu serikali ni mimi na wewe “kwahiyo naomba wale wanaoendesha vyombo vya Mamlaka na wale wanaovipanda wavitunze.”

Kikao hicho cha Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ni cha kwanza mara baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan mapema Mwezi huu.

       Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw, Reymond Mndolwa akifafanua jambo mbele ya watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji alipokuwa akizungumza nao Makao Makuu jijini Dodoma 

Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakimsikiliza Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw, Reymond Mndolwa (Hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na watumishi wa Tume hiyo Makao Makuu jijini Dodoma.

Post a Comment

Previous Post Next Post