Na. John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Rufiji. Mhe, Mohamed Mchengerwa ametoa wito kwa wananchi nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye mazoezi ya kitaifa ya uandikishaji wa anuani ya makazi na sensa yanayoendelea hivi sasa nchini kwa ajili ya maendeleo ya taifa.
Mhe, Mchengerwa ameyasema haya leo wakati akiongea na wananchi wa vijiji vya Mgomba, Ngorongo na Kilimani kwenye Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani.
Amefafanua kwamba mazoezi haya yana faida kubwa kwa nchi yetu kwa kuwa yanasaidia kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo kwa muda wa sasa na baadaye.
Aidha, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kukamilisha mipango ya maendeleo katika kipindi kifupi.
Ametaja baadhi ya mipango ambayo inatekelezwa kuwa ni pamoja na miundombinu ya barabara, shule na vituo vya afya na jengo la kujifungulia akina mama ambapo amewataka wananchi kutumia na kusimamia vizuri raslimali zinazotolewa.
Aidha ameipongeza Halmashauri ya Rufiji kwa kuwa miongoni mwa Halmashauri inayoongoza kwenye utekelezaji wa mipango ya maendeleo kupitia fedha za ndani.
"Ni jukumu lenu kuhoji kila shilingi ambayo inaletwa lakini pia kushirikiana na Serikali. Na mimi niwaahidi nitaendelea kuipigania Rufiji na mimi ni mtumwa wenu" amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Aidha, amewataka wananchi kushirikiana na Serikali katika kufanya maendeleo na kuendelea kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wanyonge.
"Tunamshukuru Mhe. Rais kwa kutujengea Shule ya Sekondari ya Bibi Titi Mohamed ambayo itatoa mchango kwa wananchi wetu". Ameongeza Mhe, Mchengerwa
Katika hatua nyingine Mhe, Mchengerwa Wizara yake inakwenda kuanza kutafuta na kuibua vipaji vya wachezaji kupitia ligi ya Samia