WAZIRI JAFO AZINDUA KAMPENI YA “SOMA NA MTI” WILAYANI TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiweka udongo kwenye mti ambao ameupanda katika uzinduzi wa Kampeni ya Soma na Mti kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo lililofanyika leo katika shule ya Sekondari Karibuni wilayani Temeke Mkoa wa Dar es Salaam. Katibu Tawala wa Manispaa ya Temeke Bi.Bupe Mwakibete akipanda mti katika uzinduzi wa Kampeni ya Soma na Mti kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo lililofanyika leo katika shule ya Sekondari Karibuni wilayani Temeke Mkoa wa Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimwagilizia maji Katibu Tawala wa Manispaa ya Temeke Bi.Bupe Mwakibete mara baada ya kupanda mti kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Soma na Mti kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo lililofanyika leo katika shule ya Sekondari Karibuni wilayani Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwamwagilizia maji wanafunzi mara baada ya kupanda mti kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Soma na Mti kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo lililofanyika katika shule ya Sekondari Karibuni wilayani Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Karibuni wakifuatilia uzinduzi wa Kampeni ya Soma na Mti kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo lililofanyika leo katika shule ya Sekondari Karibuni wilayani Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amezindua Kampeni ya “Soma na Mti” kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo lililofanyika katika shule ya Sekondari Karibuni wilayani Temeke Jijini Dar es Salaam ambapo amewataka viongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha miti iliyokusudiwa ipandwe na itunzwe.

Akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni hiyo, Waziri Jafo amesema kila halmashauri inapaswa kupanda milioni 1.5 hivyo kwa halmashauri zote 184 zinatakiwa kupanda miti 276.

Amesema lengo la kampeni hiyo ni kuchagiza ajenda ya maendeleo ya upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira nchini.

“Imani kubwa ni kwamba kama suala hili la utunzaji wa mazingira tukilipandikiza kwa wanafunzi, Taifa litafikia maeneo ambapo suala la mazingira litakuwa jambo muhimu”. Amesema Waziri Jafo.

Waziri Jafo amesema katika wilaya ya Temeke inalenga kupanda miti 71,000 kwa upande wa Shule za Sekondari pekee na kwa upande wa Shule za msingi takribani miti isiyopungua 190,000 inatarajiwa kupandwa na kwa ujumla itakuwa miti zaidi ya 260,000.

Kwa upande wake Afisa Mazingira mwanandamizi NEMC-Kanda ya Mashariki Kusini Bi.Abela Muyungi amesema kuwa miti yote tunayoipanda inatakiwa itunzwe ili itutunze kwakuwa tukipanda miti tutakuwa tunatunza mazingira na tutaboresha uhai wetu.

Pamoja na hayo amewataka wanafunzi kuendelea kuwa mabalozi wazuri katika suala la upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika ameneo yao ili mazinira yaweze kuwa safi kwa ujumla.

 Nae Katibu Tawala wa Manispaa ya Temeke Bi.Bupe Mwakibete amemuwakikishia Waziri kuwa kazi ya upandaji wa miti wataifanya kwa ushirikiano mkubwa ili lengo lililopangwa liweze kutimia.

Post a Comment

Previous Post Next Post