TBS YAENDESHA MAFUNZO YA MFUMO WA UDHIBITI UBORA NA NYARAKA ZA MAABARA

 


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Bw.David Ndibalema (katikati) akifungua Mafunzo ya siku tano ya mfumo wa Udhibiti Ubora na Nyaraka za Maabara katika Ofisi za Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam. 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Bw.David Ndibalema  akizungumza katika Mafunzo ya siku tano ya mfumo wa Udhibiti Ubora na Nyaraka za Maabara katika Ofisi za Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam. Meneja wa Mafunzo na Utafiti TBS, Mwl.Hamisi Mwanasala akizungumza katika Mafunzo ya siku tano ya mfumo wa Udhibiti Ubora na Nyaraka za Maabara katika Ofisi za Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wataalamu kutoka sekta binafsi na Umma wakifuatilia Mafunzo ya siku tano ya mfumo wa Udhibiti Ubora na Nyaraka za Maabara katika Ofisi za Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.

*******************

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewakutanisha wataalamu kutoka sekta binafsi na Umma wapatao 52 kwaajili ya Mafunzo ya siku tano ya mfumo wa Udhibiti Ubora na Nyaraka za Maabara katika Ofisi za Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Bw.David Ndibalema amesema mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha kupata elimu zaidi ya kitaalamu na kiueledi ili kuwawezesha kuwa na umahiri katika utendaji kazi kwenye maeneo yao.

Amesema kupitia mafunzo hayo yatawafanya wataalamu kuweza kutoa huduma inayoenda sambamba na matakwa ya viwango na ubora.

“Sio watu wote waliopata kujifunza kazi za maabara, mashuleni, vyuoni au kwingineko wakaweza moja kwa moja kufanya kazi kwa umahiri katika sekta za viwango na maabara”. Amesema Bw.Ndibalema.

Kwa upande wa washiriki wa mafunzo hayo wamesema matumaini yao kupitia mafunzo hayo watajifunza mambo mengi yanayogusa masuala ya maabara ili wakiwa katika majukumu yao wawe wameimarika na kuweza kuwahudumia vyema wateja wao.

Post a Comment

Previous Post Next Post