Diamond apongeza Serikali ya Rais Samia kwa kuwasaidia wasanii, kurejesha tuzo

Na. John Mapepele

Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi na  Msanii maarufu ndani na nje ya Bara la Afrika, Diamond Platinum amemshukuru  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe,  Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuwaunganisha  wasanii ili sekta ya Sanaa iweze kuwanufaisha.

Diamond amesema haya leo Machi 25, 2022 mbele ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa alipotembelea  Kampuni ya Wasafi inayomiliki rebo ya Wasafi, Wasafi TV na Wasafi FM redio kwa lengo la kukagua  kazi za Sanaa.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni imefanya mapinduzi makubwa  katika sanaa kwa  kubuni mikakati mbalimbali ya kuwaunganisha na kuwanufaisha wasanii.

Miongoni mwa mikakati ameitaja mizuri ya Serikali kuwa ni pamoja na  kurejesha tuzo za muziki.

Kwa  upande wake Mhe. Mchengerwa amesema Serikali imeshatenga  fedha nyingi kwa ajili ya kuwekeza kwenye Sanaa ili wasanii waweze kunufaika.

"Nimekuja hapa leo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yangu  ya kukutana na wadau wa sekta ninazozisimamia  ili kuwaunganisha na Serikali yao, nimefurahi kuona wasafi mnaibua vipaji na kutoa ajira kwa wasanii nchini" amepongeza Mhe Mchengerwa

Amesema  Serikali itaendelea kuwasaidia wasanii wote bila kuwabagua na kwamba Serikali inathamini mchango mkubwa unaotolewa na wasanii nchini.

Akielezea kuhusu utoaji wa burudani wa vituo vyake Diamond amefafanu kuww vinajitahidi kwenda na teknolojia ya kisasa katika kuendesha vipindi  vyenye maudhui ya kuelimisha na kuburudisha jamii.

Katika ziara hiyo, Mhe. Waziri amepata fursa ya kutembelea na kukagua shughuli za kampuni hiyo na kujionea uandaaji wa vipindi mbalimbali vya michezo na burudani vinavyotangazwa na vituo hivyo.

Mkurugenzi wa vipindi wa Wasafi  Nelson Kisanga amesema  Wasafi FM imekuwa na vipindi maarufu vya michezo vya Sports Arena na Sports  court ambavyo vimekuwa na wasikilizaji wengi.







Post a Comment

Previous Post Next Post