WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI KUFANYA MABORESHO MAKUBWA SHIRIKA LA RELI TANZANIA NA ZAMBIA (TAZARA).

 


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Atupele Mwakibete akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

………………………………………………..
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Atupele Mwakibete amesema kuwa Wizara yake itaunda Bodi Maalumu ambayo itakua inashughulikia changamoto mbalimbali zinazolikumba shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) ili kulifanya lifanye kazi kwa ufanisi mkuwa.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam wakati alipotembelea shirika hilo na kufanya mazungumzo na na watendaji na wafanyakazi wa shirika pamoja na kukagua kalakana ya kukarabati vitu mbalimbali ikiwemo injini na mabehewa.

Naibu Waziri Mwakibete amesema kuwa shirika hilo linakumbwa na changamoto malimbali ikiwemo uchakavu wa miundombinu , madeni makubwa ya wafanyakazi hali ambayo inachangia shirika kushindwa kujiendesha kwa ufanisi mkubwa.

Amesema kuwa serikali ya Tanzania na Zambia zimeanza kufanya mchakato wa kubadilisha sheria ili kufanya marekebisho, kwani sheria iliyopo kwa sasa inazuia kufanya uwekezaji wowote upande wa Tanzania bila kukubaliana na serikali ya zambia.

“Tunashindwa hata kuendeleza upande wetu wa serikali kwa sababu sheria iliyopo inazuia kuwekeza chochote katika reli hii mpaka tukubaliane na wenzetu, hivyo tayari mchakato wa kubadilisha sheria hii unaendelea tukikamilisha hata baadhi ya changamoto zitapungua ”amesema Naibu Waziri Mhe. Mwakibete.

Ameongeza kuwa baadhi ya wafanyakazi wa TAZARA hawapewi mikataba ya kudumu ya ajira hali ambayo inawafanya wakose morali ya kufanya kazi, huku akisema kuwa suala hilo linafanyiwa kazi na serikali.

Meneja Mkuu wa TAZARA Tanzania Fuad Abdallah, amesema kuwa shirika hilo linakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uchakavu wa miundombinu, upungufu wa mabehewa na injini ,madeni ya wafanyakazi, madeni ya mifuko ya kijamii pamoja na madeni ya wasanbazaji .

“Shirika hili limanzishawa mwaka 1976 ni miaka 42 sasa lilianzishwa likiwa na injini 106, lakini kwa sasa tuna injini 14 pekee ni changamoto tuna upungufu mkuwa wa injini na mabehewa “ amesema

Post a Comment

Previous Post Next Post