TANAPA YAZINDUA ZAO JIPYA LA UTALII JIJINI ARUSHA,WADAU WENGI WAUNGA MKONO

 Na Pamela Mollel,Arusha


Shirika la hifadhi za Taifa Tanzania(Tanapa)limezindua zao jipya la utalii linalohusu mbio ambazo zinafanyika ndani ya hifadhi ya Taifa ya Arusha (Anapa)lenye jina la Arusha Park Wildlife Marathon kwa lengo la kukuza utalii pamoja na kutangaza vivutio mbalimbali

Kwa mara ya kwanza tarehe 20 Februari 2022 mbio hizo za riadha zimetimua vumbi katika hifadhi ya Arusha National Park huku washiriki takribani 70 kutoka vilabu vya Arusha na Moshi

Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Biashara Beatrice Kessy wakati akizindua mbio hzo alisema kuwa utalii na michezo vimeweza kuungana pamoja jambo ambalo limepelekea washiriki vijana kuwa wengi ukilinganisha na wazee

"Sisi kama shirika la hifadhi Tanzania hatuna budi kuanzisha michezo ya aina mbalimbali katika hifadhi za Taifa ili tuwavutie vijana wengi zaidi"alisema Kessy

Alisema mbio za Marathon zimekuwa maarufu sanaa hapa Tanzania lakini pia Dunia kote hivyo imekuwa fursa ya mazao ya utalii katika hifadhi ya Arusha

"Hifadhi hii ipo karibu sana na mji wa Arusha hivyo tukaona Arusha,Moshi na miji mingine jirani inawapenzi wengi wa kukimbia mbio hizi za Marathon "alisema Kessy

Kupitia zao hilo jipya la utalii litawezesha vijana kushiriki kwa wingi jambo ambalo pia watafanya utalii wa ndani kupitia michezo

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa hifadhi ya Arusha Albert Mziray alisema mbio hizo zinatarajiwa kufanyika November mwaka huu

"Mbio hizi zitafanyika mwezi wa kumi na moja mwaka huu zitakuwa mbio kubwa kweli kweli tutegemee mambo makubwa zaidi"alisema Mziray

Alisema kuwa kupitia mazao mapya ya utalii ikiwemo utalii wa magari ya zamani pamoja na mbio za utalii zimewavutia watalii wa ndani na nje hivyo wamejipanga kuongeza zao lingine la upandaji wa mlima Meru kwa kutumia baskeli

"Usalama upo wa kutosha ndani ya hifadhi hakuna mkimbiaji atakayepata shida kwa kuwa askari wetu wapo kila kona kuhakikisha usalama"alisema Mziray

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Richard Luyango ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwapongeza waandaaji pamoja na washiriki wa mbio hizo kwa kuweza kupata washiri 70walioweza kukimbia mbio hizo

"Kama taifa tunapaswa kumshkuru Mungu kwa kutupa eneo kama hili lenye utajiri mkubwa, kwa nchi za wenzetu mbuga kama hii kwao ni ya kitaifa"alisema Luyango

Naibu Kamishna uhifadhi mahusiano Tanapa Catharine Mbena alisema kuwa wataendelea kuwa wabunifu katika kubuni mazao mapya ya utalii ili watalii wote wanaokuja kutalii katika hifadhi zetu wakute vionjo sambamba na ubora wa bidhaa pamoja na huduma

Pia aliweka wazi faida zinazopatikana kupitia mbio hizo ni pamoja na kuendelea kuboresha afya na kufurahia utalii

Mratibu wa mbio hizo Lomayan Komolo alisema lengo la mbio hizo ni kujenga uelewa ndani ya jamii nzima kuhusu hifadhi ya Arusha pamoja na vivutio vyake

Mshiriki wa mbio hizo Baraka Mallya(Fresh Coach)kutoka Moshi alisema mbio hizo zimefana sana kwa ambao hawakufanikiwa kufika wamekosa kitu kikubwa na cha kihistoria.


Picha ikionyesha washiriki wa mbio za Arusha Park Wildlife Marathon wakitimua vumbi katika hifadhi ya Taifa ya Arusha National  Park ikiwa ni zao jipya la utalii katika hifadhi hiyo

Kamishna Msaidizi wa hifadhi ya Arusha Albert Mziray akikimbia mbio katika hifadhi ya Taifa Arusha national park
Kamishna Msaidizi maendeleo ya biashara Beatrice Kessy  akikimbia riadha katika hifadhi ya Arusha,zilizozinduliwa rasmi leo tarehe 20 Februari 2022
Naibu Kamishna uhifadhi mahusiano Tanapa Catharine Mbena akikimbia riadha katika hifadhi ya Arusha national park

Mwakilishi wa Arusha Club Ibrahim Komba akipokea zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Arumeru Richard Luyango

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Richard  Luyango akizungumza na washiriki mara baada ya mbio hizo kukamilika ambapo aliwapongeza kwa ushiriki wao katika mbio hizo.

Post a Comment

Previous Post Next Post