NAIBU WAZIRI KASEKENYA AKAGUA DARAJA LA BUBUTOLE WILAYANI CHEMBA

 

Kazi za utoaji wa mawe chini ya Daraja la chuma la Bubutole lenye urefu wa mita 60 ili kuruhusu maji kupita vizuri na kwa wingi zikiendelea wilayani Chemba, mkoani Dodoma. Daraja hilo la chuma limefungwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) mara baada ya daraja la zamani kukatika kutokana ongezeko la maji mengi yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo hayo na mkoa wa Manyara.

Muonekano wa Daraja la chuma la Bubutole lenye urefu wa mita 60 lililofungwa na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), wilayani Chemba, Mkoani Dodoma.

 


 

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Godfrey Kasekenya (kulia), akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng.  John Temu, wakati alipokuwa akikagua Daraja la chuma la Bubutole lenye urefu wa mita 60 lililofungwa na Wakala huo ili kufungua mawasiliano ya barabara ya Zamahero – Kinyamshindo (km 124.6), Wilayani chemba, mkoani Dodoma

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Godfrey Kasekenya (kulia), akiongozana na Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng. John Temu, wakikagua Daraja la chuma la Bubutole lenye urefu wa mita 60 lililofungwa na Wakala huo, mara baada ya daraja la zamani kukatika na kufunga mawasiliano ya barabara inayoanzia Zamahero – Kinyamshindo (km 124.6), katika Wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma

Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng. John Temu, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Godfrey Kasekenya, wakati akikagua kazi iliyofanywa na Wakala huo ya ufungaji wa Daraja la Chuma mara baada ya daraja la zamani la Mto Bubu kukatika na kusimamisha shughuli za usafirishaji katika Wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma

Post a Comment

Previous Post Next Post