NCAA Yatoa Mafunzo Kwa Wanahabari Arusha Kuhusu Utalii W A Urithi Wa Utamaduni

 Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imetoa mafunzo ya Siku moja kwa Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Arusha kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu utalii wa Urithi wa utamaduni na Mambo Kale


Akitoa mada katika mafunzo hayo Kamishna Msaidizi Mwandamizi anayesimamia Idara ya Urithi wa Utamaduni na Jiolojia Eng. Joshua Mwankunda ameeleza kuwa Ngorongoro ni eneo lenye utalii wa Vivutio vingi ikijumuisha utalii wa mambo kale,  Jiolojia, nyayo za binadamu wa kale, bonde la Olduvai na kambi ya waanaakiolojia  maarufu duniani Dkt. Louis na Merry Leakey.

Eng. Mwankunda amebainisha kuwa eneo la Ngorongoro ndio sehemu yenye ushahidi pekee duniani unaolezea historia ya binadamu wa kale duniani pamoja na gunduzi mbalimbali kwa ufasaha na ushahidi usio na mashaka

“Eneo la Ngorongoro ndio sehemu yenye gunduzi mbalimbali za historia ya binadamu, binadamu kusimama na miguu yake miwili, ugunduzi wa fuvu la binadamu wa kale duniani “zinjathropus” na hata sasa zipo tafiti mbalimbali zinazoendelea katika bonde la Olduvai" ameafafanua Eng Mwankunda

Amewaeleza wanahabari hao kuwa kutokana na utajiri wa rasilimali hizo zilizoipa hifadhi Ngorongoro Sifa mbalimbali duniani za kiuhifadhi ndio maana UNESCO ilitambua eneo hilo kama urithi wa Dunia.

Kwa upande Kamishna Msaidizi Mwandamizi anayesemamia Uhusiano wa Umma Joyce Mgaya ameeleza kuwa Mafunzo kwa wanahabari ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa NCAA kutoa uelewa wa bidhaa mbalimbali za utalii zilizopo katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ili kusaidia kuelimisha jamii juu ya uwepo wa fursa hizo.

Kaimu Kamishna Msaidizi Mwandamizi- Uhusiano wa Umma NCAA Joyce Mgaya akizungumza na Wanahabari wa Mkoa wa Arusha wakati wa mafunzo kwa wanahabari hao
Kaimu Kamishna Msaidizi Mwandamizi- Uhusiano wa Umma NCAA Joyce Mgaya akizungumza na Wanahabari wa Mkoa wa Arusha wakati wa mafunzo kwa wanahabari hao
Kamishna Msaidizi Mwandamizi (Urithi wa Utamaduni na Jiolojia) Mhandisi Joshua Mwankunda akitoa mada wakati wa mafunzo ya Wanahabari mkoani Arusha
Wanahabari wakifuatilia mada

Post a Comment

Previous Post Next Post