WALIMU WATAKIWA KUTOA USHAWISHI KWA WANAWAKE KUPENDA MASOMO YA SAYANSI

 **************************

Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Philibert Luhunga amesema hivi sasa dunia inakabiliwa na majanga mawili,ambayo ni Uviko 19 na Mabadiliko ya Tabia nchi,kikubwa ni mwanamke kuweza kupambana na changamoto zinazoikabili jamii.

Ameyasema hayo leo wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuazimisha siku ya wanawake wanaosoma Sayansi Duniani iliyofanyika katika katika ofisi za COSTECH Jijini Dar es Salaam.

“Masuala ya mabadiliko ya tabia nchi ni janga ambalo Dunia inapitia,hivyo wanawake wanapaswa kujikita kusoma masomo ya Sayansi kutafuta namna ya kupambana na changamoto hizo zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi”. Amesema.

Kwa upande wake mbobezi wa masuala ya Sayansi Dkt. Hulda Gidion amesema tunahitaji kupata wanasayansi wengi ili kuunda usawa wa kijinsia pia kuleta mabadiliko kwenye jamii.

Amesema somo la Sayansi ni muhimu kutokana na kwamba linambinu nyingi za kutatua changamoto za masuala mbalimbali yanayoikumba jamii kwa ujumla




Post a Comment

Previous Post Next Post