YAKUBU- VYUO VIKUU ENDELEENI KUANDAA MATAMASHA

 Na. John Mapepele

Naibu Katibu Mkuu wa Utamaduni, sanaa na Michezo. Saidi Yakubu ametoa wito  kwa vyuo vikuu nchini vinavyofundisha sanaa kuandaa matamashaa  ya utamaduni ili kuibua vipaji vitakavyoleta ajira kwa vijana.

Yakubu ameyasema  haya  leo  Januari 29, 2022 alipokuwa akimwakilisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed  Mchengerwa wakati wa kilele cha tamasha la  sanaa la kuadhimisha miaka 60 ya Chuo  Kikuu cha Dar es Salaam toka kuanzishwa kwake.

Amefafanua kwamba matamasha haya yanasaidia kuibua vipaji na kuendeleza utamaduni wa taifa letu.

Aidha, amesema Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa nafasi ya washindi watatu katika tamasha hili kushiriki kwenye tamasha kubwa la kitaifa la Serengeti litakalofanyika  Dodoma mapema mwezi Machi 2022.

Amekipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa  kuunga  mkono juhudi za Mhe. Rais katika kuendeleza Utamaduni na dira yake ya 2061 na mikakati yake ya kuimarisha utamaduni wa ubunifu ndani ya Chuo.

Ametaja baadhi ya ubunifu  huo kuwa ni pamoja na  kuanzisha kozi zinazodumisha ubunifu na kuchochea  uzalendo  kwa ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.

Amesema  kuwa utamaduni, sanaa na michezo ni maeneo muhimu katika maisha ya wananchi ambapo amefafanua kuwa faida ya kuenzi utamaduni ni kuwa unatusaidia kutumia ujuzi, taaluma na teknolojia ya jadi na  kisasa katika kuimarisha afya,rasilimali na kuleta tija kwa ujumla.

Katika shindano hilo Rodney Rutashorwa amekuwa mshindi wa kwanza na kujinyakulia shilingi milioni na Yusufu Mkoma akichukua nafasi ya pili na kupata shilingi laki sana na  nafasi ya tatu ikienda kwa Moses Selestine aliyeibuka na kitita cha shilingi la laki tank.






Post a Comment

Previous Post Next Post