MAMLAKA ya Mapato Tanzania ( TRA ) kwa kushirikiana na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) wameanza kamapeni ya elimu kwa mlipakodi mlango kwa mlango Zanzibar kisiwan Unguja ambayo litafanyika Kwa muda wa siku tano kuanzia tarehe 4/12/2021 hadi 8/12/2021.
Kampeni inalenga kutoa elimu kwa walipakodi ili kuwajengea uelewa wa kutosha juu ya maswala mbalimbali yanayohusu kodi, kusikiliza maoni yao kwa ajili ya kuboresha huduma za kikodi, Kuwakumbusha kulipa kodi stahiki na kwa wakati kuskiliza kero na changamoto walizonazo na hatimaye kuzitafutia ufumbuzi.
Zoezi hilo lilifunguliwa rasmi tarehe 4/12/2021 na Naibu Kamishna wa TRA Zanzibar Juma Bakari Hassan tarehe 4/12/2021 ambapo katika ufunguzi huo aliongelea maswala mbali mbali ikiwemo kutatua changamoto za wafanyabiashara waliotembelewa na kuweza kupata taarifa sahihi Kwa ajili kusajiliwa Kwa wale ambao hawajasajiliwa
Vilevile aliwahiimiza maofisa wa TRA kutumia lugha nzuri na kuwaelemisha walipakodi kwa ufasaha juu ya wajibu na haki zao , kuzingatia weledi uwajibikaji na uadilifu pia awashukuru viongozi wa ngazi mbali mbali wa Serikali ya Zanzibar Kwa ushirikiano waliotoa katika maandalizi na utekelezaji wa zoezi la Elimu ya kodi mlango kwa mlango.