Mkuu wa mkoa kaskazini Unguja Mh. Ayoub Mohamed MahmoudMkuu wa mkoa wa kaskazini Unguja pamoja na Maofisa wa TRA na ZRB
****************
Maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA wakishirikiana na Bodi ya Mapato Zanzibar – ZRB walifanya Mazungumzo na Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Mh. ayoub Mohamed Mahmoud na kuwashukuru TRA na ZRB Kwa kufika katika Mkoa wake 6/12/2021.
Aidha Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud amewaomba Wafanyabiashara kulipa kodi Kwa hiari Kwa maendeleo ya nchi vilevile nakutoa agizo Kwaupande wa uongozi wa serekali za mitaa masheha na Baraza la miji kila mwenye uhitaji wa leseni ya biashara afike TRA kwanza kupata Tax clearance kabla kupatiwa leseni hiyo ya biashara hii itasaidia serekali kukusanya kodi.
Pia Mkuu wa Mkoa Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud amewashukuru TRA na ZRB Kwa kuweza kufika katika Mkoa wake na kutoa elimu ya kodi mlango Kwa mlango na kuwaomba wawavute wafanyabiashara hasa Kwa upande wa utalii na uvuvi ili jukumu lao Kwa serekali liweze kutekelezwa