NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara,akizungumza kwenye Ofisi ya Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Barabara ya Mzunguko katika jiji la Dodoma yenye kilomita 112.3 kabla ya kuanza ziara ya kukagua ujenzi huo.
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara,akimsikiliza Meneja TANROARDS Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu kwenye Ofisi ya Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Barabara ya Mzunguko katika jiji la Dodoma yenye kilomita 112.3.
Wakandarasi wakifatilia hotuba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara,(hayupo pichani) kwenye Ofisi ya Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Barabara ya Mzunguko katika jiji la Dodoma yenye kilomita 112.3.
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara,akimsikiliza Meneja TANROARDS Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu akimuonyesha mchoro wa Mradi wa Barabara ya Mzunguko katika jiji la Dodoma yenye kilomita 112.3.
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara,akitoa maelekezo kwa Meneja TANROARDS Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu mara baada ya kuonyeshwa mchoro wa Mradi wa Barabara ya Mzunguko katika jiji la Dodoma yenye kilomita 112.3.
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara,akiendelea na ziara ya kukagua ujenzi wa Mradi wa Barabara ya Mzunguko katika jiji la Dodoma yenye kilomita 112.3.
Muonekano wa Mradi wa Barabara ya Mzunguko katika jiji la Dodoma yenye kilomita 112.3.
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara,akizungumza mara baada ya kumaliza ziara yake ya kukagua Mradi wa Barabara ya Mzunguko katika jiji la Dodoma yenye kilomita 112.3.
Meneja TANROARDS Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu,akisisitiza ujenzi wa Mradi wa Barabara ya Mzunguko katika jiji la Dodoma yenye kilomita 112.3.
……………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Mwita Waitara ameuagiza Wakala wa Barabara Nchini(TANROARDS) kuhakikisha wanashughulikia changamoto ya madai ya dalili za kudaiwa rushwa kwa vijana wanaoomba kufanya kazi kwenye mradi wa Barabara ya Mzunguko katika jiji la Dodoma yenye kilomita 112.3.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa Barabara ya Mzunguko katika jiji la Dodoma yenye kilomita 112.3.
“Nimetumiwa meseji kuwa wakati mnachukua vijana kufanya kazi hapa kuna malalamiko yanatolewa kuwa kuna dalili za rushwa ili wapate kazi hivyo sisi kama Serikali hatutaki kusikia hilo kwenye kazi hivyo angalieni kwenye eneo hili maana linachafua taswira ya eneo hili,”.
“Rais aliagiza wanaozunguka miradi wapewe kazi kama wana vigezo bila kuzungushwa hivyo wakianza kusema wamedaiwa rushwa inachafuka kampuni na kama hilo lipo likome na wapewe kazi kama wanafaa badala ya kuwa na tuhuma za rushwa hivyo mnaosimamia fanyeni kazi kwa weledi,” amesemaa Waitara.
Alibainisha kuwa mradi huo ni mzuri wenye manufaa kwa wananchi sababu utapunguza msongamano hivyo ukikamilika utafungua njia ya Dodoma na kuondoa upotoshaji kuwa hautafanyika.
“Mmeshalipwa asilimia 20 ya fedha hadi sasa hivyo chapeni kazi kwa mujibu wa mkataba ambao unaeleza hadi Desemba 7, 2024 uwe umekamilika hivyo mkiweza malizeni kabla ya muda. Viongozi wataendelea kuja hapa mara kwa mara sababu Serikali imewekeza fedha nyingi hivyo hakikisheni mnalipa fedha kwa kadri mlivyoingia mkataba sio kuwazungusha,”amesema
Kwa upande wake Meneja TANROARDS Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu amesema mradi huo ulianza Septemba mwaka huu na utatekelezwa ndani ya miezi 79.
Mhandisi Chimagu amesema kuwa kiasi cha sh. bilioni 12.47 zimelipwa kama fidia kwa wananchi 2.388 waliopisha mradi ambapo kati ya hao 470 waliobaki wanaendelea kulipwa sababu fedha zimeshatolewa wiki iliyopita.