TAMASHA LA KIHISTORIA LATUA MBEYA-BASHUNGWA

 

Na. John Mapepele, WUSM

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Filamu nchini inatarajia kwa mara ya kwanza tangu Tanzania kupata uhuru wake kufanya tamasha kubwa la kihistoria la utoaji wa tuzo mbalimbali za filamu ambalo litafanyika Disemba 18, 2021 jijini Mbeya.

Akizungumza na kwenye Mkutano wa Waandishi wa   wa habari jijini Mbeya, Novemba 29, 2021 Mhe. Bashungwa amesema sababu kubwa ya kufanyia kilele cha tuzo hizi jijini Mbeya ni kutambua uwepo wa wanatasnia ya filamu pamoja na wasanii katika mikoa na maeneo mengine nje ya Dar es Salaam ili kuamsha ari ya kufanya kazi za sanaa na hatimaye kujipatia ajira na kipato kitakacho boresha maisha yao.

  “Tamasha hili linakwenda kufungua milango ya fursa mbalimbali zilizoko maeneo hayo katika uwanja huu wa filamu na Sanaa kwa ujumla kupitia idadi kubwa ya wapenzi wa filamu watakaokuwa wanafuatilia tukio hili ndani na ncje ya nchi yetu.”. Amefafanua

Aidha amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, imedhamilia kuleta mapinduzi makubwa kwenye tasnia ya sanaa na Filamu ndyo maana imekuwa na miokakati mbalimbali ya kuboresha tasnia hiyo  ikiwa ni pamoja na kutoa tuzo za filamu kwa wanatasnia ya filamu hapa nchini kwa lengo la kutambua mchango wa wahatasnia hao.

“Kwa mwaka huu wa fedha, Mhe. Rais ametenga kiasi cha Sh. Bilioni 1.5 kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni ambao niliuzindua tarehe 22 Novemba 2021. Mfuko huo utatoa mikopo na kuwezesha programu mbalimbali za kuendeleza Sanaa nchini ikiwemo filamu” amefafanua Mhe. Bashungwa

Akifafanua zaidi Mhe. Bashungwa amesema  katika  kuboresha  kazi za sanaa na Filamu nchini Novemba 22,  2021, alizindua  Mfumo wa kidijitali utakaokuwa unatumiwa na Taasisi za BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA, ambazo ziko chini ya Wizara yake.

Ametaja baadhi ya faida za mifumo hiyo kuwa ni pamoja na kurahisha utendaji wa Taasisi hizo katika kuwahudumia wasanii kwa kutia huduma kwa haraka,kuwarahisishia wasanii wote nchini na hata nje ya nchi kupata huduma kokote walipo bila kufika katika ofisi hizo, ambazo ni BASATA, BODI YA FILAMU na COSOTA na kutunza kumbukumbu za wasanii na kuleta wepesi wa kuwatambua kokote walipo ili kurahisisha utoaji huduma kwao kama vile mafunzo mbalimbali ya Sanaa ambayo Taasisi hizi zimekuwa zikiyatoa.

“Huu ni wakati muafaka wa kuonyesha nguvu na mchango mkubwa wa Tasnia ya Filamu katika kuchochea ukuaji wa Uchumi. Sekta ya burudani inayohusisha filamu imefanya vizuri katika nyanja za Kiuchumi, kwa mfano, mnamo mwaka 2018 Sekta hii iliongoza kwa ukuaji wa kasi ya zaidi ya 13%, ambapo ilishika nafasi ya tatu mwaka 2019 kwa ukuaji wa kasi ya 11%. “ amesisitiza Mhe. Bashungwa

Post a Comment

Previous Post Next Post