RAIS SAMIA AMETENGA SH. 1.5 BILIONI KWA MFUKO WA MAENDELEO YA SANAA NA UTAMADUNI-WAZIRI BASHUNGWA

 Waziri wa Tamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Innocent Bashungwa (katikati) akizindua Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika leo katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Tamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Innocent Bashungwa akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC leo Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Tamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Pauline Gekul akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC leo Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wa Zanzibar Mhe.. Tabia Mwita kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC leo Jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Tamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania Bw.Yusuph Singo akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni nchini Dkt.Emmanuel Temu akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC  leo Jijini Dar es Salaam. Wadau mbalimbali wa Tamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika leo katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam. Msanii wa Kizazi Kipya Saraphina akitoa burudani kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC leo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**********************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Tamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Innocent Bashungwa amesema Rais  Mheshimiwa Samia Suluhu ametenga shilingi bilioni 1.5 kwa Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni  na kutoa wito kwa wadau wengine kuchangia mfuko huo.

Ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Mifumo ya Kidigitali ya BASATA, Bodi ya Filamu na COSOTA na Mashindano ya Samia Taifa Cup, uliofanyika katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam.

Amesema mfuko lazima uanze sasa kuwasaidia wadau wenye ubunifu katika mawazo yatakayoonekana ni mazuri, tuyachambue vizuri, na kuwapa mikopo kwa lengo la kutekeleza mawazo hayo.

“Wasanii na wadau wengine wameteseka sana, kila kitu kwenda mguu kwa mguu kufika ofisini kupata itatuzi. Nimpongeze Katibu Mkuu Dkt. Abbasi, na timu nzima ya wakuu wa taasisi hizi kwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao (Ega) kuratibu na kushirikiana kujenga mifumo hii. Kuanzia leo wasanii na wadau watapata huduma wakiwa popote kutokea kiganjani mwao”. Amesema Waziri Bashungwa.

Pamoja na hayo Mhe.Bashungwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita imekusudia kufufua michuano ya Taifa Cup, na kuiendeleza ili iweze kufikia malengo yake ya kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo nchini, hasa kwa kuwapa nafasi zaidi wanamichezo na wasanii walioko mikoani.

“Napenda kuwaeleza kuwa kwenye mashindano ya mwaka huu tunaanza na michezo mitatu kwa kuanzia, ambayo ni soka kwa wanaume na wanawake, netiboli kwa wanawake, na riadha kwa wanaume na wanawake. Mashindano haya yamepangwa kuanza tarehe 10 – 16/12/2021 katika viwanja vya Benjamin Mkapa, Uhuru na uwanja wa ndani wa Taifa”. Amesema.

Kwa Upande wake Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo wa Zanzibar Bi. Tabia Mwita amesema kuwa anapongeza ushirikiano uliopo baina ya serikali hizi mbili.“Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiana katika mambo haya kama la usajili kwa kutumia mfumo wa kidigitali na kuanza rasmi kwa Samia Taifa CUP kuwa yanaonesha umoja wetu kwa vitendo.” 

Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Tamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa itawapa nafasi wasanii kupeleka maombi yao huko na yatapatiwa majibu.

“Uzinduzi wa Bodi hii leo unatoa nafasi ya mfuko huu kufanya kazi yake vizuri na upya ambao kwa hakika utawezesha wadau kupata mikopo na mafunzo na kusahau yaliyopita”. Amesema 

Post a Comment

Previous Post Next Post