MAAGIZO YA NAIBU WAZIRI BASHE KWA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI

 

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akizungumza na
wahandisi wa Umwagiliaji wa Mikoa nchini hawapo pichani Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya  Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Profesa Henri Mahoo,
akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri Bashe na Wahandisi wa
Umwagiliaji wa Mikoa nchini hawapo pichani

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Daudi Kaali
akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri Bashe na wahandisi wa
Umwagiliaji wa Mikoa nchini.

Sehemu ya washiriki wa kikao, cha Naibu Waziri Bashe jijini Dodoma.

Na; MwandishiWetu -Dodoma

Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe. Hussein Bashe (MB) ameiagiza Tume ya
Taifa ya Umwagiliaji kupitia wahandisi wa wake wa mikoa kuainisha eneo
linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, na kusema kuwa ni ngumu  kuwa na
kilimo endelevu cha umwagiliaji kama hakuna mfumo endelevu wa kilimo
hicho.

Naibu Waziri  Bashe,ameyasema hayo Jijini Dodoma,
alipokuwa katika kikao cha pamoja na wahandisi wa Umwagiliaji wa Mikoa
na menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Bashe alise
makuwa, wahandisi wa Umwagiliaji nchini wanatakiwa kwenda kusajili skimu
zote za kilimo ilikuweza kupata picha halisi,na kuzitambua skimu hizo
pamoja na eneo lote linalofaa katika kilimo cha umwagiliaji.

“Potential
areas za miradi zitambulike, na za mabwawa zitambulike, tutenganishe
miradi inayoweza kufanywa kwa ujenzi shirikishi yaani force account na
miradi mingine.” AlisisitizaBashe.

Aliendelea kusema kuwa, ni
Lazima Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ijue inajenga hekta ngapi mpya za
Umwagiliaji, pamoja na kuzifanyia matengenezo skimu nyingine, na
kujiekea malengo ilikuweza kufikia lengo la ilani ya Chama cha Mapinduzi
inayotaka hekta zaidi ya milioni moja na laki
mbili(1,200,000)kumwagiliwa ifikapo mwaka 2025.

Akiongea kuhusu
Mitambo iliyopo katika sekta ya kilimo cha  Umwagiliaji na kumilikiwa na
Tume ya Taifa yaUmwagiliaji, Naibu Waziri Bashe alisema, vifaa vyote
vifanyiwe matengenezo na uanishwe ununuaji wa mitambo mipya.

Awali
Naibu Waziri Bashe,aliagiza Tume hiyo kuwa na Muundo katika sekta ya
kilimo cha umwagiliaji utakaoonesha wahandisi wa umwagiliaji wa Wilaya
nchini na alisisitiza swala zima la kuandaa budget halisi itakayokidhi
mahitaji ya Ofisi hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post