Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakichukuwa chakula wakati wa futari ya pamoja iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Magonjwa ya Moyo jana jijini Dar es Salaam. Kila mwaka wakati wa mwezi wa mfungo wa Ramadhan Kurugenzi tano za Taasisi hiyo zinaandaa futari kwa nyakati tofauti kwa ajili ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo. Futari hiyo ilidhaminiwa na kampuni ya Samiro ambao ni waagizaji na wasambazaji wa dawa za binadamu.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakila futari iliyoandaliwa na Kurugenzi ya Magonjwa ya Moyo jana jijini Dar es Salaam. Kila mwaka wakati wa mwezi wa mfungo wa Ramadhan Kurugenzi tano za Taasisi hiyo zinaandaa futari kwa nyakati tofauti kwa ajili ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo. Futari hiyo ilidhaminiwa na kampuni ya Samiro ambao ni waagizaji na wasambazaji wa dawa za binadamu.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Magonjwa ya Moyo ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo Tatizo Waane akimsikiliza Abbas Mohammed ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Samiro ambao ni waagizaji na wasambazaji wa dawa za binadamu wakati wa futari ya pamoja iliyoandaliwa kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo.
Picha na JKCI