NAIBU WAZIRI KIPANGA AWAAGIZA WATUMISHI WIZARA NA VIONGOZI WA TAASISI KUTEKELEZA MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA

 

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkataba wa huduma kwa wateja uliofanyika leo  Mei 6,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mkataba wa huduma kwa wateja iliyofanyika leo Mei 6,2021 jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo, Moshi Kabengwe,akitoa maelezo mafupi kuhusu hafla ya uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Wateja uliozinduliwa leo Mei 6,2021 jijini Dodoma.
Watendaji, Watumishi wa Wizara ya Elimu na wadau wa wizara hiyo wakimfuatilia Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa mkataba wa huduma kwa wateja iliyofanyika leo Mei 6,2021 jijini Dodoma .
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Leonard Akwilapo kitabu cha mkataba wa huduma kwa wateja uliozinduliwa leo Mei 6,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Dkt. Charles Msonde,akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga (hayupo pichani) mara baada ya kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja iliyofanyika leo Mei 6,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Omar Kipanga amewaagiza watumishi, wakuu wa idara, vitengo na wakuu wa vyuo vilivyo chini ya Wizara hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia weredi wa taaluma zao sambamba na kufuata miiko ya kazi zao na taaluma zao.

Maagizo hayo ameyatoa leo Mei 6,2021 jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mkataba wa huduma kwa wateja katika Wizara hiyo , amesema hawata sita kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa watakaoshindwa kutekeleza kajukumu yao kikamilifu kwa mujibu wa mwongozo wa mkataba huo.

“Niwaagize watumishi wote wa Wizara,Wakuu wa Idara na Vitengo, Wakuu wa vyuo mfanye kazi kwa kuzingatia taaluma zenu ili mkataba wa huduma kwa mteja utekelezwe kwa viwango vinavyotarajiwa

“Mkataba utatumika kama njia ya mawasiliano na wateja wetu, na sisi Wizara tutahakikisha tunatoa huduma bora na za kuridhisha kuhakikisha tunafikia lengo la serikali”amesema Kipanga.

Pia Mhe.Kipanga ameagiza taasisi zote zilizochini ya Wizara ya elimu kuhakikisha kila taasisi ina mkataba wa huduma kwa mteja kulingana na mwongozo wa utekelezaji wa mkataba huo.

“Mhakikishe mna mikataba iliyohai na mnatekeleza kwa viwango vinavyotakiwa, na taasisi zenye mikataba iliyopitwa na wakati ihuwishwe ili kuendana na wakati” amesema.

Aidha amewaasa viongozi wateuliwa kuwasimamia watumishi ili kutoa huduma bora kwa wateja na kwamba Wizara itawapongeza viongozi na watumishi watakaofanya vizuri.

 “Ufanisi katika utekelezaji wa mkataba huu hautaletwa na viongozi na watumishi wa wizara pekee bali utategemea ushirikiano wa wadau wote wa wizara, hivyo niwaombe wadau wote kutoa ushirikiano thabiti kwa Wizara ili kuhudumiwa kwa ubora na viwango tulivyoahidi”amesema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo, amesema utekelezaji wa mkataba huo utafungua ukurasa mpya wa uwajibikaji kwenye maeneo ya kazi na kuleta tija iliyotarajiwa.

 “Kuna mambo mengi tumetoa ahadi bungeni na tutakuwa na mjadala mkubwa kwa ajili ya mstakabali wa elimu yetu, tujipange kwa hili pia”amesisitiza

Awali Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo, Moshi Kabengwe, amebainisha kuwa ili kuhakikisha mkataba unafanya kazi kwa ufanisi, Wizara imeandaa fomu maalum ambayo itaonesha mrejesho wa huduma alizopata mteja kama ameridhika nayo au la.

Amesema Wizara imechapisha vitabu 6000 vya mkataba huo ambavyo vitasambazwa kwenye taasisi zote za wizara ambao utatoa dira ya utoaji huduma katika taasisi zilizochini ya Wizara ya Elimu sayansi na Teknolojia

Post a Comment

Previous Post Next Post