Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,akizungumza wakati akifunga warsha ya siku mbili kwa Watumishi wa REA,Wahandisi na Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato,akizungumza na Watumishi wa REA,Wahandisi na Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati akifunga warsha ya siku mbili kwa Watumishi wa REA,Wahandisi na Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa umeme vijijini (Rea) Mhandisi Advera Mwijage,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki baada ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani kufunga warsha ya siku mbili kwa Watumishi wa REA,Wahandisi na Mameneja wa TANESCO Mkoa na Kanda ulikuwa na lengo lakutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini uliofanyika jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali imeagiza kuvunjwa kwa bodi ya manunuzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wao kwa kuwa na malalamiko mengi katika suala la manunuzi.
Agizo hilo limetolewa Jijini Dodoma na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Medard Kalemani,wakati akifunga mkutano uliowakutanisha REA na TANESCO ,Wahandisi na Mameneja wa Mikoa ulikuwa na lengo la kutathimini utekelezaji wa miradi ya usambazaji Nishati Vijijini.
Dkt. Kalemani amesema bodi hiyo ya manunuzi imekuwa ikipigiwa kelele sana kutokana na ukilitimba uliopo katika suala la manunuzi kwa kukiuka kanuni za manunuzi.
“Lazima bodi hii ivunjwe kuanzia leo hii na ichaguliwe nyingine na ianze kazi leo hii manake kumekuwa na ukilitimba mkubwa sana katika manunuzi, anaachwa mtu mwenye bei ndogo katika manunuzi na kuchukuliwa mtu mwenye bei juu hii sio sawa” amesema Dkt. Kalemani
Mbali na kuvunjwa kwa bodi hiyo Waziri Kalemani ameagiza uchunguzi ufanyike kwa wahusika wote walikuwa wakilalamikiwa juu ya ukiukwaji wa sheria za manunuzi katika bodi na wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Dkt. Kalemani amewaagiza mameneja wote wa TANESCO hapa nchini kuhakikisha wanaongeza kasi ya usambazaji wa umeme katika maeneo mbalimbali yaliyosalia.
“Azma ya serikali ni huduma hii ya umeme kufikia vijiji vyote vilivyosalia ifikapo Desemba 2022, hivyo kuanzia sasa tunamiezi 18, kukamilisha zoezi hili ili kuvifikia vijiji vyote vilivyo baki ambaye hatafikia lengo hata vumilika kabisa” amesema.
Aidha Dk. Kalemani amepiga marufuku mgao wa umeme na ukataji wa umeme bila kutoa taarifa kwa wananchi na atakaye shindwa kutimiza hilo ataipoteza nafasi yake mara moja.
“Pamoja na suala la mgao wa umeme na kukatika kwa umeme lakini pia meneja ambaye atashindwa kuwaunganishia umeme wananchi ambao wamelipia kwa wakati hatua kali zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuondolewa katika nafasi yake”amesisitiza
Hata hivyo Dkt.Kalemani amesema pamoja na kuongezeka kwa ukusanyaji wa mapato lazima TANESCO waongeze jitihada zaidi katika suala la ukusanyaji na matumizi sahihi ya fedha za Serikali.
“Ukusanyaji mapato miaka ya nyuma ulikua bilioni 9, kwa wiki, mwaka juzi ukawa bilioni 36 kwa wiki mwaka jana bilioni 39 kwa wiki lakini hivi sasa ni takribani bilioni 46 kwa wiki hivyo mnatakiwa kuongeza juhudi ikibidi tuwazidi hata TRA” amesema.
Katika hatua nyingine Dkt. Kalemani amesema kuwa, Serikali imeridhishwa na utendaji kazi wa Watumishi wa REA ,Wafanyakazi wa TANESCO na Wizara ya Nishati imekuwa ikijivunia utendaji kazi wao.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa umeme vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage, amesema kuwa watahakikisha maagizo yote yaliyotolewa na Waziri wanayafanyia kazi ili wananchi wote wanufaike na Nishati hiyo ya umeme