MALIASILI NA UTALII WATEKELEZA AGIZO LA RAIS SAMIA

 

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhe Ludovick Nduhiye akihutubia wakati wa ufunguzi wa KIJIJI SOKO, Kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam

Balozi wa Marekani nchini Mhe Don Wright  akitia sahihi katika bango la Kijiji Soko kama sehemu ya kumbu kumbu ya kuudhuria kwakwe.

*******************************

Na Sixmund J. Begashe

Wizara ya Maliasili na Utalii nchini, imezindua rasmi program maalumu ijulikanayo kama KIJIJISOKO kupitia Kijiji cha Makumbusho ili kutoa fursa kwa wasanii wa sanaa za ufundi nchini kuonesha kazi zao na kuziuza ili kuongeza pato la taifa na binafsi pamoja na kuwavutia watalii kununua mazao ya utamaduni sehemu moja.

Akifungua Maonesho hayo kwa niamba ya Katibu Mkuu wa Malialisi na Utalii, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Ludovick Nduhiye ameeleza kuwa mkakati huu ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan la kuwainua wasanii kiuchumi na kuimarisha sekta ya utalii nchini.

Bw. Nduhiye amesisitiza kuwa Wizara ya Maliasili itaendelea kuboresha mazingira ya utalii nchini hasa kwa kujenga soko la kisasa la mazao ya utamani kama sanaa za ufundi katika Kijiji cha Makumbusho ili wasanii nchini waweze kuuza kazi zao lakini pia watalii wasipate usumbufu wa kutafuta kazi hizo bali watazipata sehemu moja na kwa wasanii wenyewe.

Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga amesema kuwa ofisi yake, imejipanga kikamilifu kushirikiana na wadau mbali mbali ili kuendeleza urithi wa kiutamaduni hususan sanaa ambayo ni moja ya mazao muhimu ya utamadini nchini ili Taifa linufaike na kazi za wasanii kwa kupata watalii wengi wa ndani na nje ya nchi.

“Ilani ya Chama tawala imetuelekeza, kuendeleza urithi wa kiutamaduni na Mambo Kale pamoja na kuvitangaza vivutio hivyo ili kuvutia watalii wengi zaidi lakini pia kushirikiana na wadau mbali mbali katika kuhakikisha dhima hii ya Serikali inafikiwa”. Amesema Dkt. Lwoga.

“Mhe Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kalisisitizia hilo hivyo. sisi tumeona tulitekeleze kwa kupitia program mbali mbali ikiwepo hii ya Kijiji Soko” Aliongeza Dkt Lwoga

Balozi wa Marekani nchini Mhe Don Wright  licha ya kuipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kuanzisha KIJIJI SOKO ameeleza kuwa program hiyo itakuwa ni kivutio kikubwa kwa watalii wanaotoka Marekani na kuahidi kuendelea kuunga mkono jitihada hizo huku Balozi wa Ujerumani nchini Mhe  Regina Hess amesema kuna raia wengi wa Kijerumani nchini pamoja na watalii wanaoingia nchini itakuwa ni rahisi kwao kujipatia bidhaa za wasanii kupitia Kijiji Soko

Akizungumza kwa niaba ya wasanii wa Sanaa za Ufundi nchini, Rais wa Sirikisho hilo (TAFCA) Bw Adrian Nyagamale  ameishukuru na kuipongeza Serikali kupitia Makumbusho ya Taifa kwa kuwashika mkono wasanii kupitia KIJIJI SOKO kwani kwa kupitia program hii wasanii wengi watainuka kiuchumi na imewatia moyo wasanii waliokata tamaa ya kutengeneza kazi za Sanaa.

“Serikali imetusaidia pakubwa sana, kazi zetu ni mazao ya utamaduni wetu, hivyo nitoe wito kwa jamii kupenda kununua kazi za wasanii wa hapa nchini, kwanza ni imara na zinavutia ukilinganisha na zile za nje, watanzania sasa watumie Kijiji Soko kujipatia kazi za wasanii maana hapa watawakuta wasanii wenyewe wengine wakiendelea na kazi za Uchongaji”. Aliongeza Bw Nyangamale

Post a Comment

Previous Post Next Post