Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja (Wa kwanza kulia) akiwa pamoja na Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na Viongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) wakikagua maeneo mbalimbali ya ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la (JNHPP-MW2115) wakati wa ziara ya viongozi hao ya kukagua eneo ambalo miti yake inatakiwa kung’olewa ili kupisha ujenzi wa Bwawa la maji kwa ajili ya kufua Umeme.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja, Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na baadhi ya viongozi wa Taasisi za Uhifadhi za Wizara ya Maliasili na Utalii wakiangalia kazi inayoendelea ya ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme wakati wa ziara ya kamati hiyo ya kukagua Hifadhi ya Taifa ya Nyerere pamoja kuangalia zoezi la ung’oaji wa miti katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi ya Maliasi na Utalii, Dkt. Aloyce Kwezi (wapili kulia) akielezea umuhimu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha inaweka vivutio vya Utalii vitakavyo zunguka eneo la Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere pindi litakapokamilika ili kuvutia wageni wengi zaidi wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Hifadhi ya Taifa ya Nyerere mkoani Morogoro. Wa pili Kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja, Kamishna wa Uhifadhi, Prof. Dos Santos Silayo ( wa kwanza kushoto) na wajumbe wengine walioshiriki katika ziara hiyo