WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YATEKELEZA AGIZO LA RAIS WA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN P. MAGUFULI.

 

  1. Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Viwanda, Wizara ya Viwanda na Biashara Mhandisi Ramson Mwilangali (wa kwanza kulia) akizungumza katika kikao cha Mkuu wa Wilaya ya Kasulu na Mwekezaji aliyeonesha nia ya kuwekeza kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda.

Mkurugenzi Mkazi wa kampuni ya Agroprocessing Tz Ltd ndugu Dhaval Maheshwari akifuatilia kwa makini kikao kati ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, wakilishi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Eneo huru la Uwekezaji (EPZA) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kujadili uwekezaji wa eneo la kilimo cha mpunga na ujenzi wa kiwanda.

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Kanali Simon Anange akizungumza wakati wa kikao na mwekezaji aliyeonesha nia ya kuwekeza kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha Sukali.

Baadhi ya wataalamu kutoka taasisi za serikali wakiwa na mwekezaji katika shamba lenye ukubwa wa hekta 37,662 lililotengwa maalumu kwa ajili ya uwekezaji wa kilimo cha miwa na Halmashauri ya wilaya ya kasulu.

Baadhi ya wataalamu kutoka taasisi za serikali wakiangalia ramani ya shamba kumuonesha mwekezaji mwenye nia ya kuanzisha kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari.

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa kampuni ya Agroprocessing Tz Ltd ndugu Dhaval Maheshwari

***************************************

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mhe. Kanali Simon Anange pamoja na Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu Mhe. Joseph Kashushura, Tarehe 3 Machi, 2021 wamepokea ujumbe kutoka wizara ya Viwanda na Biashara, EPZA, TIC na Bodi ya Sukari ulioambatana na mwakilishi mkazi wa kampuni ya Mahashree Agroprocessing Tz Ltd mwenye nia ya kuwekeza kiwanda cha sukari na kilimo cha miwa.

Ziara hii imekuja mara baada ya agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John P. Magufuli aliyoitoa tarehe 12 Februari, 2021 alipokuwa akizindua kiwanda cha nafaka cha Mahashree Agroprocessing Tz Ltd kilichopo Mkoani Morogoro.

Mhe. Rais aliiagiza Wizara ya viwanda na Biashara kwa kushirikiana na EPZ na TIC kuhakikisha wanampatia mwekezaji ambaye ni Mahashree Agroprocessing Tz Ltd eneo zuri kwa ajili ya kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari ili kuongeza uzalishaji wa sukari nchini, kuleta ajira na kodi kwa serikali.

Katika kutekeleza agizo hilo la Rais, Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekazaji (TIC) ilifanya jitihada za upatikanaji wa shamba ambalo linapakana na mto Malagalasi lenye ukubwa wa hekta 37,662. Shamba hili lipo katika kata tatu za Heru Ushingo, Kitanga na Nyamidaho zenye vijiji saba ambavyo ni Nyarugusu, Kiyungwe, Kitanga, Kumtundu, Nyamidaho, Kigadye na Heru Ushingo.

Baada ya kuzungunguka na Mkurugenzi Mkazi wa kampuni ya Mahashree ndugu Dhaval Maheshwari katika eneo la mradi ambalo lipo umbali wa kilometa 70 hadi 110 kutoka Makao makuu ya Wilaya ya Kasulu.

Mwakilishi huyu wa mwekezaji alivutiwa zaidi na shamba hili ambapo amesema kuwa kwa sasa watafanya upembuzi yakinifu ya ardhi na wakishakamilisha wataanza na kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari ambapo kwa kiasi kikubwa watahusisha wanakijiji wanaozunguka eneo la mradi kushiriki pia katika kilimo cha miwa (Out Growers) kwa ajili ya malighafi ya kiwanda.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilzaya ya Kasulu Mhe. Kanali Simon Anange amepogeza jitihada zinazofanywa na Wizara ya Viwanda na Biashara, TIC, EPZA na Bodi ya Sukari (SBT) kwa kulichagua eneo la Kasulu kuwa kitovu cha uwekezaji kwa kumleta mwekezaji ambaye ameonesha nia ya kuwekeza katika kilimo cha miwa na ujenzi wa kiwanda cha sukari.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amefanya mazungumzo na mwakilishi wa mwekezaji na kumhakikishia ushirikiano wa kila hatua ili kuhakikisha uwekezaji huu mkubwa unaanza mapema kwani Kigoma ni eneo zuri la uwekezaji hasa ukizingatia uwepo wa mto malagalasi ambao unatiririsha maji ya kutosha na uwepo wa reli kwa ajili ya usafirishaji wa mashine za kiwanda na bidhaa.

Post a Comment

Previous Post Next Post