Waziri wa
Maji Jumaa Aweso amesema hawezi kumuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisononeka kwa wananchi wa mijini na
Vijijini wakikosa maji.
Hayo ameyasema wakati wa ziara ya
kutembelea Viwanda hivyo vya uzalishaji wa mabomba iliyofanyika leo
Jijini Dar es Salaam kwa kutembelea kiwanda cha Simba Pipe na Plasco.
Aweso
amewahakikishia Viwanda vya utengenezaji na usambazaji wa mabomba ya
maji kuwa changamoto zote zitafanyiwa kazi ili sekta ya maji kufika
mbele zaidi kwa kuwa na ushirikiano wa pamoja.
Akizungumza kwa
nyakati tofauti na Viwanda vya Simba na Plasco vyote vinavyozalisha
mabomba ya uzalishaji wa mabomba ya kusafirishia maji, Aweso amesema
viwanda vya ndani vitaendelea kutoa huduma kwa miradi yote ya serikali
kwa usawa.
Amesema, Wizara ya maji inatakiwa kuendeleza mahusiano
mazuri na wadau wa sekta ya maji wakishirikiana kwa pamoja na kutakuwa
na kikao kikubwa sana baina ya serikali na viwanda vinavyozalisha vifaa
vinavyotumika kwenye miradi ya maji.
"Hatutaki kuona viwanda
wanashirikiana na vishoka kwani wao ndo wanakwamisha miradi mingi ya
maji kukwama na kuwataka watumie njia sahihi ya kupata tenda za
usambazaji wa mabomba ya maji kwenye miradi inayoendelea takribani
miradi 651," amesema
Aidha, amewataka viwanda hivyo kuanza
kutengeneza pampu za kusukumia maji na kulikua na kisingizio kutoka kwa
wataalamu kuhusiana na usambazaji wa mabomba kwenye miradi ila amejionea
mwenyewe na kusiwe na kisingizio chochote kwa sasa.
Aweso
amesema, changamoto ya malipo kwa wakati itafanyiwa kazi kwa sababu wote
wanataka kutoa huduma kwa wananchi na watahakikisha malipo yanafanyiwa
kwa kazi na kulipwa kwa wakati ili kazi ziweze kuendelea na miradi
kukamilika kwa wakati.
Mkurugenzi wa Manunuzi wa Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Hellen Lupogo
amesema wamekuwa na ushirikiano mzuri wa viwanda vya uzalishaji mabomba
ikiwemo Plasco na Simba Pipe na ziara hii itazidisha mahusiano mazuri
Kati ya Mamlaka za maji na viwanda hivi.
Amesema, viwanda hivyo
vimekuwa vinafanya kazi zake kwa wakati na hata Afisa Mtendaji Mkuu wa
Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja alishatembelea na kufanya mazungumzo
wa viwanda hivi ili kuboresha mahusiano mazuri ya kibiashara.
Naye
kwa Upande wa Wakala na Usambazajiw a Maji Vijijini (RUWASA) Mhandisi
Clemence Kivegelo amesema kuna changamoto mbalimbali ambazo wameweza
kuzipokea kutoka katika Viwanda vya uzalishaji wa mabomba ya kusambazia
maji na wameshaanza kuzifanyia kazi.
Amesema, tayari wameshakaa
na TRA na Wizara ya Fedha ili kuangalia msamaha wa kodi (Tax Extansion)
kwa viwanda vinavyosambaza mabomba ya kusambazia maji ambapo unaweza
kukuta mradi ni wa miaka miwili ila msamaha unatolewa kwa mwezi mmoja
Mkurugenzi
Mtendaji wa Simba Pipe Jitin Pratap Singh amesema wamejipanga katika
kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wateja wao hususani Mamlaka zote za
maji zinazochukua mabomba kutoka kwao wakiwemo RUWASA na DAWASA.
Amesema,
Simba Pipe imeweka mkakati wa kuunda application katika mtandao ili
mafundi wanapokuwa kazini kusoma kwa umakini namna ya kufunga mabomba
kwani unapokosea kuunga sehemu moja unakuwa umeharibu mfumo mzima.
"Tunaunga
mkono juhudi za serikali za kutimiza adhma ya Rais Dkt John Pombe
Magufuli za Tanzania ya Viwanda na Wizara ya maji ya kumtua Mama Ndoo
Kichwani," amesema
Aidha, ameongezea na kusema kwa sasa
wanazalisha tani 18,000 kwa mwaka kwa mabomba ya HDPE na UPVC na pia ni
kiwanda cha kwanza kuzalisha mabomba ya Gesi nchini.
Hata hivyo
kwa upande wa kiwanda cha Afisa Uendeshaji wa Kiwanda cha Plasco,
Alimiya Osman amesema wanafurahi kutembelewa na Waziri wa Maji Jumaa
Aweso na Uongozi mzima wa RUWASA na DAWASA na wataendelea kushiriana kwa
ukaribu zaidi.
Amesema kwa sasa wanazalisha malighafi za tani 28,000 kwa mwaka na katika tani hizo ni asilimia 70 ni mabomba ya HDPE.
Mkurugenzi wa Manunuzi DAWASA Hellen Lupogo akieleza jambo kwa Waziri wa Maji Jumaa Aweso vinavyozalisha mabomba hayo yanayotumika katika miradi mbalimbali ya maji nchini. Waziri aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clemence Kivegele na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe.
Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clemence Kivegele akielezea namna Viwanda vya Simba Pipe na Plasco vinavyofanya kazi kwa ukaribu mkubwa na Mamlaka za maji kwa ajili ya mabomba yanakusafirisha na kusambaza maji. Waziri Aweso alifanya ziara ya kutembelea viwanda hivyo leo Jijini Dar es Salaam