WAZIRI MKUU AZINDUA MWONGOZO WA UWEKEZAJI MKOANI SINGIDA

 

WAZIRI
anayeshughulikia Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Singida kulia ni Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na katikati ni Katibu Tawala wa
Mkoa wa Singida Angelina Lutambi

 

WAZIRI anayeshughulikia Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Singida kulia ni Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi na katikati ni Katibu Tawala wa
Mkoa wa Singida Angelina Lutambi

Kikundi cha Ngoma Asili cha Sarakasi wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Mwongozo huo

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi mwenye kilemba cheupe akishiriki kucheza ngoma ya asilina wadau mbalimbali



WAZIRI wa Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akikagua baadhi bidhaa zilizoletwa na wadau mbalimbali

Kwaya ya Chuo cha Utumishi Singida wakitumbuiza wakati wa tukio hilo
Na John Mapepele, Singida

Waziri
kuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassimu Majaliwa 
amezitaka  Mamlaka zote za Mikoa  kujipanga kikamilifu kutangaza fursa
za uwekezaji zinapatikana kwenye  mikoa yao kwa kushirikiana Kituo cha 
Taifa  cha Uwezekezaji  ili kuhakikisha kuwa fursa zote zilizoainishwa
kwenye  miongozo ya  uwekezaji  zinapata wawekezaji makini ili kuongeza 
mapato na ajira kwa wananchi

 Akisoma  hotuba  ya Mheshimiwa
Waziri Mkuu kwenye  tukio la uzinduzi wa Mwongozo wa Fursa za Uwekezaji
Mkoa wa Singida,   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uwekezaji Profesa Kitila
Mkumbo amesema kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo  wa miaka  mitano(5)
Serikali imedhamilia  kuimarisha  ustawi wa wananchi wake  kwa kuzalisha
ajira  milioni nane na kukuza uchumi wake kwa asilimia nane  hivyo
uwekezaji  makini unatakiwa ili kufanikisha azma hiyo.

Amesema 
ili kuwapata wawekezaji makaini watendaji wote wa Serikali hawana budi
kutoa taarifa sahihi za fursa zinazopatikana  katika maeneo yao na
utaratibu wote wa namna ya  kuufuata ili kuweza kuwekeza.

“Ndugu
zangu ni muhimu sana tubadilike  taarifa za uwekekezaji tunazozitoa
ziwe  sahihi na ziwe zinafanana, ukienda kwa Mkuu wa  Mkoa upate taarifa
sawa na ukichukua taarifa hiyo kwa  Katibu Tawala wa Mkoa na Mkurugenzi
Mtendaji wa  Halmashauri hapo tutakuwa tumefanikiwa” amesisitiza
Profesa Mkumbo.

Amezitaka  mamlaka hizo kutowakwamisha 
wawekezaji kwa  kuhakikisha  maeneo ya uwekezaji  yanapatikana mara moja
ili pindi Wawekezaji wanapofika wanapatiwa   maeneo hayo na
wanahudumiwa  kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto zozote
zinazojitokeza.

Amesema  balozi  namba moja  anayeweza kuleta au
kutoleta wawekezazi katika nchi yoyote  duniani ni Muwekezaji aliye
ndani ya nchi husika  hivyo  ni muhimu  kuwapa huduma  bora  ili waweze
kutuletea wawekezaji wengi zaidi ambapo amesisitiza  uwekezaji ufanywe
kwa kuzingatia sheria, taratibu na miongozo ya  Serikali ili nchi yetu
iweze kunufaika.

Amekemea tabia  ya kupenda kutoa lawama  baada
ya  kuingia mikataba  mibovu na wawekezaji na badala yake amewataka 
watendaji kuwa makini katika  mchakato mzima wa majadiliano na kufunga
mikataba hiyo na wawekezaji.

Aidha, ameitaka  kila Mkoa kuangalia
kuangalia maeneo  machache ya kipekee ili kufanya uwekezaji  wenye tija
badala ya kwenda na maeneo mengi ambayo  hayana  tija.

Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ameishukuru
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais John Pombe
Magufuli kwa kubuni mikkakati  kabambe ya uwekezaji ambayotayari katika
kipindi kifupi imeleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kijamii kwenye
nchi yetu.

Amesema Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa ambayo
ilikuwa ikionekana kama  mikoa masikini lakini sasa  umekuwa  ni
miongoni mwa mikoa ambayo inaweza kuongoza  kuleta  mapato makubwa kwa
nchi  kutokana na  kuboreshwa kwa  mazingira na fursa nyingi zilizopo.

Ametaja
baadhi ya fursa za uwekezaji  zinazopatikana kuwa ni pamoja na madini,
kilimo  cha Alizeti na Korosho, mafuta asilina na gesi pia elimu.

Post a Comment

Previous Post Next Post