TANESCO YAKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA KUSAFIRISHA NA KUPOZA UMEME WA SGR DAR-MORO

 

Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya njia za  kusafirisha Umeme na vituo vya kupokelea na kupoza umeme wa Reli ya SGR kutoka Kinyerezi Dar es salaam Mpaka mkoani Morogoro umekamilika.

Mhandisi Albano Sembua kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) leo amesema ujenzi wa miundombinu hiyo umekamilika kwa asilimia 99% kazi iliyobaki ni kuunganisha umeme huo ili kuanza kazi ambapo gharama za ujenzi ni shilingi za kitanzania bilioni 71.1.

Mhandisi Sembua amesema hayo mbele ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliotembelea na kujionea utekelezaji wa mradi huo katika eneo la Kinguruwira mkoani Morogoro ambapo pia watashiriki semina iliyoandaliwa na shirika la umeme la (TANESCO) na kutembelea mradi mkubwa wa kimkakati wa ujenzi wa Bwawa la kufua umemela Julius Nyerere Hydro Power Project. litakalozalisha megawati 2115.

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bi. Grace Kisyombe katikati akiwa ameongozana na baadhi ya wahariri kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakati walipotembelea ujenzi wa Miundombinu ya Kusafirisha na kufua umeme katika mradi wa SGR eneo la Kinguruwira mkoani Morogoro.

Mtangazaji wa Kituo cha Redia cha Clouds Masoud Kipanya akiongozana na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Majira Bw. Emannuel Mbuguni wakati wahariri walipotembelea mradi wa ujenzi wa vituo vya kupoza umeme katika njia ya Reli ya Umeme SGR mkoani Morogoro.

Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakitembelea mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na vituo vya kupoza umeme katika Reli ya umeme SGR katika eneo la Kinguruwira mkoani Morogoro.

Miundombinu ya kituo cha kupokelea  na kupoza umeme wa Reli ya SGR eneo la Kinguruwira mkoani Morogoro kinavyoonekana mara baada ya ujenzi wake kukamilika.

Post a Comment

Previous Post Next Post