Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia) akizungumza na Menejimenti ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kuhakikisha wanahamasisha utalii wa ndani ili kuongeza Watalii wakati wa kikao kilichofanyika mapema leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akiongoza Kikao na Menejimenti ya Bodi ya Utalii Tanzania kilichofanayika leo Jijini Dar es Salaama. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devota Mdachi
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Mary Masanja (wapili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TEHAMA na TAKWIMU wa TTB, Rossan Mduma (wa kwanza kulia) kuhusu Studio ya Kidijitali itakayotumika kutangaza na kukusanya taarifa mbalimbali za kidijitali zinazohusiana na Bodi hiyo mara baada ya kikao na Menejimenti ya Bodi hiyo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa TTB Bi. Devotha Mdachi na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Shirika, Bi. Monica Mahenge.
…………………………………………………………………….
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja leo tarehe 22 Feb, 2021 akiwa Jijini Dar es Salaam amefanya Kikao na Menejimenti ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kujadili masuala mbalimbali ikiwemo kutumia siku za maadhimisho na matukio mbalimbali yanayofanyika ndani ya Tanzania kutangaza na kuhamasisha utalii wa ndani . Aidha, Mhe. Masanja ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha inaendelea na jitihada za kuhamasisha Utalii kwa kasi na kuongeza ubunifu wa kutangaza vivutio vya utalii nchini ili kutimiza matakwa ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) ya mwaka 2020-2025