Wizara ya Maji yamtaka Meneja RUWASA Mbeya kukamilisha miradi ya maji haraka.

 

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akishiriki ujenzi wa tenki la maji mkoani Mbeya

 Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza na wananchi katika chanzo cha maji cha mradi wa maji Mwakaleli wilayani Rungwe Mkoani Mbeya

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca mahundi akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila alipotembelea ofisini kwake wakati wa ziara yake mkoani hapo.

************************************************

Na Evaristy Masuha.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amemuagiza Meneja wa Wakala wa Usambazaji maji Vijijini mkoa wa Mbeya Mhandisi Hans Patrick Kuhakikisha anakamilisha mradi wa maji wa Mwakaleli ifakapo Februali 28, mwaka 2021.

Mhandisi Mahundi alitoa agizo hilo jana alipotembelea na kukagua miradi ya maji katika ziara ya siku moja ambayo pia alitumia kuzungumza na wananchi.

 Naibu Waziri amesema mradi wa maji wa Mwakaleli ambao umekuwa ukisuasua kukamilika kwa muda mrefu unatakiwa kukamilika haraka ili wananchi  waanze kupata huduma ya majisafi na salama huku akitoa mwezi mmoja kwa meneja huyo kuwasilisha andiko la ukamilishaji wa mradi wa maji unaotegemea maji kutoka chanzo cha Nyara, ili taratibu za haraka zifanyike na wananchi waanze kupata huduma ya maji.

Vilevile Naibu Waziri amemuagiza Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira  Mbeya Mhandisi Ndele Mengo kuhakikisha anatatua changamoto ya huduma ya maji katika mji wa Tukuyu ambao umekuwa ukipata maji kwa mgao.

Amesema hakuna sababu yoyote ya kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi hiyo kwani serikali imetoa fedha takribani shilingi Bilioni 1.7  kwa ajili ya mradi wa Mwakaleli. Lakini pia imenunua pampu ambayo itaondoa tatizo la kusafirisha maji kwa wananchi wanaotegemea mradi wa Masoko.

” Niwahakikishie wananchi kuwa maji yatafika katika maeneo yote hivyo musiwe na wasiwasi,” Waziri Mahundi aliwawahakikishia wananchi. 

 Amesema wilaya ya Rungwe ina vyanzo vya maji vya kutosheleza vijiji vingi. Kwahiyo ni wajibu wa wataalamu kuhakikisha huduma hiyo inafikishwa kwa wananchi.

Post a Comment

Previous Post Next Post