WIZARA YA KILIMO KUANZISHA DAWATI MAALUMU KUSIKILIZA KERO ZA WAWEKEZAJI SEKTA BINAFSI

 

Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda akizungumza kwenye kikao cha wadau wa zao la ngano kilichofanyika jijini Dodoma leo Januari 23,2021 ambapo  Wizara imeingia makubaliano na makampuni makubwa ya ngano ikiwemo Bakhresa, Azania, Sunkist, AMSONS,Jumbo, TBL na Serengeti Breweries kuanza kununua ngano ya wakulima wa kwa bei ya shilingi 800 kwa kilo.

Baadhi ya washiriki wa kikao cha wadau wa ngano wakimsikiliza Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda(hayupo pichani) wakati  akizungumza kwenye kikao cha wadau wa zao la ngano kilichofanyika jijini Dodoma leo Januari 23,2021 ambapo  Wizara imeingia makubaliano na makampuni makubwa ya ngano ikiwemo Bakhresa, Azania, Sunkist, AMSONS,Jumbo, TBL na Serengeti Breweries kuanza kununua ngano ya wakulima wa kwa bei ya shilingi 800 kwa kilo.

Waziri wa Kilimo Prof.Adolf Mkenda  akisisitiza jambo kwenye kikao cha wadau wa zao la ngano kilichofanyika jijini Dodoma leo Januari 23,2021 ambapo  Wizara imeingia makubaliano na makampuni makubwa ya ngano ikiwemo Bakhresa, Azania, Sunkist, AMSONS,Jumbo, TBL na Serengeti Breweries kuanza kununua ngano ya wakulima wa kwa bei ya shilingi 800 kwa kilo.

Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akizungumza kwenye  kikao cha wadau wa zao la ngano kilichofanyika leo jijini Dodoma Januari 23,2021 ambapo Wizara imeingia makubaliano na makampuni makubwa ya ngano ikiwemo Bakhresa, Azania, Sunkist, AMSONS,Jumbo, TBL na Serengeti Breweries kuanza kununua ngano ya wakulima wa kwa bei ya shilingi 800 kwa kilo.

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya akizungumza wakati wa kikoa cha wadau wa ngano kilichofanyika leo jijini Dodoma Januari 23,2021.

………………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Katika kuhakikisha inamaliza kero za wawekezaji nchini  Wizara ya Kilimo ipo mbioni kuanzisha dawati maalumu litakalotumika na sekta binafsi katika kuwasilisha kero zinazowakabili katika shughuli zao.

Hayo yamebainishwa leo Januari 23,2021 jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo Profesa  Adolf Mkenda wakati wa kikao cha wadau wa zao la ngano amesema kuwa  katika dawati hilo wataweka watu makini watakaoweza kutatua kero za wawekezaji nchini.

“Tutaliimarisha dawati hilo kikamilifu na watu tutakaowaweka ni watu makini kweli kweli ambao watakuwa na uwezo wa kushughulikia kero za wakulima na wawekezaji katika sekta ya kilimo” amesema Prof. Mkenda.

Amesema Wizara ya kilimo imejizatiti kikamilifu kuhakikisha wanafanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kutazama zao moja baada ya jingine ili kuhakikisha kero katika mazao hayo zinaondoshwa.

Amesema serikali imeweka mikakati ya kuliamsha tena zao la ngano na shayiri ili kupunguza kuagizi mazao hayo kutoka nje ya nchi, ambapo uzalishaji wa ndani ukiwa ni tani 60,000 hadi 70,000 licha ya wataalam kusema Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuzalisha ngano katika nchi za Afrika Mashariki.

Prof. Mkenda amesema kadri mda unavyo songa mbele wakulima wamekuwa wakiacha kulima ngano kutokana na  kutumia gharama nyingi lakini bei yake bado ikiwa chini.

Amesema kama Serikali wemekuwa wakifanya kila jitihada kuhakikisha uzalishaji unaongezeka kutoka kuzalisha tani 0. 7 hadi tani 1 kwa ekari moja ya ngano hadi kufikia uzalishaji wa nje ambao huzalisha hadi tani 5 kwa ekari moja.

Ameongeza kuwa “Bei iko chini wakulima hawana hamasa na kiwango cha ubora kiko chini, tusipoyamaliza haya kilimo hakitakuwa endelevu, leo tunaanza safari ya kunyanyua tena zao la ngano na shayiri, kwa ngano bei tumepandisha hadi kufikia 800” amesema.

Aidha amewataka wakulima wa ngano waliochukua mashamba ya serikali kuhakikisha wanalima mashamba hayo kabla serikali haijachukua uamuzi mwingine kwani kama mwanzo zao hilo lilisahaulika lakini sasa watalisimamia kikamilifu.

“Wenye mashamba ya serikali walime ngano au tunayachukua hatupendi kutuma ishara ya aina yoyote kwao,” amesema.

mewataka sekta binafsi kuangalia namna ya kuwaunganisha wakulima wenye mashamba madogo madogo ili kujiunga kwenye mfumo wa ushirika ili waweze kuzalisha ngano nyingi.

Pia amesema makubaliano mengine walioingiua na wenye viwanda ni kuwa, wanaoagiza ngano watanunua ngano kutoka ndani, wakinunua asilimia 60 ya ngano ya nje watanunua asilimia 60 ili kuipa soko ngano inayozalishwa ndani inayozalishwa ndani,

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,  Gerald Kusaya amesema kuwa Tanzania imekuwa ikitumia trioni 1.03 kwa ajili ya kuagiza ngano kutoka nje ya nchi.

“Tanzania ina hekta milioni 44 zinazofaa kwa kilimo lakini ni hekta milioni 10.8 ndio zinatumika inafika sehemu tunaagiza ngano hii ni aibu haifai kuifumbia macho” amesema Kusaya.

Yodas Mwanakwatwe yeye ni Meneja wa kanda wa kati wa Benki ya Kilimo Tanzania , amesema mabenki ya kilimo yatafungua fursa nyingi kwenye kilimo, usindikaji na usafirishaji .

Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara (TPSF), Dk Godwin Kiwanga , amesema kilimo cha ngano kitasaidia katika kukuza uchumi na kitaleta ajira.

“Tunahitaji uchumi kukua na kwa asilimia nane hadi 10 na kilimo kitasaidia kuongeza ajira,” alisema.

Amesema suala la ardhi linatakiwa kupewa umuhimu wa kutosha ili kuingia katika kilimo cha mkataba,

Pia kuwe na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuendesha kilimo.

“Wewekezaji wa sekta binafsi wahakikishe wanaweka viwanda vya kuchakata ngano kabla ya kuuza na kuhakikisha teknolojia ya kilimo inaweza kuenea kwa watu wengi zaidi na kuboresha mazingira ya biashara ili kuweza kwenda mbele,” amesema.

Post a Comment

Previous Post Next Post