Woinde Shizza ,ARUSHA
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) wafanya bonanza la michezo mbalimbali jijini Arusha katika maadhimisho ya mapinduzi ya Zanzibar ili kupunguza msongo wa mawazo ya ukusanyaji Kodi lakini pia kuwaleta kwa pamoja watumishi.
Akizungumza wakati wakiendelea na michezo mbalimbali Kamishna mkuu wa TRA Edwin Mhede amesema kuwa kazi zao zimekuwa na changamoto kubwa katika ukusanyaji wa Kodi hivyo michezo itawasaidia kubadilishana mawazo na kujadili mambo mbalimbali .
" Michezo ni afya ,michezo ni undungu hivyo tukikutana tukajumuika kwa pamoja katika sikukuu hii ya kitaifa ili tutakaporudi kazini tuwe na afya njema "
Aidha amesema kuwa kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni kuhamasisha wafanyabiashara kutumia mashine ya EFD pamoja na wananchi kudai risiti pindi wanaponunua bidhaa ili kuhakikisha wanapata bidhaa zenye uaminifu .
Mhede amesema lengo la kufanya bonanza hilo katika mkoa wa Arusha
kwa sababu wako kwenye majadiliano ya mikakati ya nusu mwaka jijini humo .
Aidha aliwaagiza kila viongozi wa TRA kila mkoa kuandaa simu ya bonanza Katika mkoa wake na wasifanye Mara moja moja bali wawe wanafanya mabonanza ya wafanyakazi wa mamlaka hiyo kila Mara kwani michezo inaongeza ufanisi Katika utendaji kazi wao.
Bonanza hilo limefanyika katika viwanja vya chuo cha uhasibu IAA wakijuhusisha na michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, Pete ,vikapu kuruka kamba pamoja na kufukuza kuku.
Naye meneja utawala TRA Yasin Mwita ameeleza namna michezo itakavyo wasaidia kuwa wakakamavu katika suhala zima la ukusanyaji Kodi kwani wanafanyakazi kwa muda mrefu hivyo mazoezi Yana umuhimu kwao.
" Tunakazi nyingi Sana ambazo zinatupelekea kuwa na changamoto hivyo michezo hii ina umuhimu kwetu ili tuweze kukabiliana na changamoto zilizopo katika kazi zetu"
Kwa upande wake meneja wa TRA mkoa wa Songwe Farence Mniko amefurahia maazimisho hayo yaliyofanyika kwa kutumia michezo mbalimbali kwani wametengeneza mahusiano mazuri na wafanyakazi walioko mikoa mbalimbali kwa kubadilishana ujuzi.