Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara akiwasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi mkoani humo kwa ajili ya kukagua shughuli za mazingira katika miradi mbalimbali.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara akikagua mradi wa dampo la taka ngumu katika eneo la lililopo katika Halmashauri ya Mji wa Geita mkoani Geita.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara akitoa maelekezo alipokagua mradi wa dampo la taka ngumu katika Halmashauri ya Mji wa Geita mkoani Geita.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara akikagua bwawa la majitaka lililopo mradi wa dampo la taka ngumu katika eneo la lililopo Halmashauri ya Mji wa Geita mkoani Geita.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
************************************************
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara ametoa wiki mbili kwa Ofisi ya Mkoa wa Geita kufanya ukaguzi kuhusu mradi wa dampo la taka ngumu kutokana na kujengwa chini ya kiwango tofauti na gharama halisi.
Waitara ametoa maagizo hayo leo Desemba 28, 2020 alipofanya ziara katika eneo la mradi huo uliopo katika Halmashauri ya Mji wa Geita ambao umetumia takriban sh. bilioni 1.9 huku ukiwa bado haujakamilika wala kukabidhi kwa Halmashauri hiyo.
Alisema Serikali hautawavumilia wanaokwamisha miradi na kusababisha hasara na kuagiza mkandarasi huyo atafutwe na arudishwe katika eneo hilo ili akamilishe mradi au arudihe fedha.
“Katibu Tawala wa Mkoa naagiza mfanye ukaguzi ndani ya wiki mbili tumpate mchawi wa mazingira na mnipe ripoti nani alihusika, nani alisaini mkataba, fedha zilitumikaje, alilipwa nani na kwa kazi kazi, hatuwezi kuvumilia vitendo hivi, hii ni hujuma kwa Serikali,” alionya.
Akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Afisa Mazingira wa Mji wa Geita, Albert Kashaga alisema yapo mapungufu yaliyojitokeza yakiwemo ujenzi wa kisima kimoja cha kufanya ufuatiliaji badala ya vitatu kwa mujibu wa mkataba.
Mapungufu mengine ni kutokuwepo kwa mitambo ya kuendeshea dampo wala mzani wa chini kwa ajili ya kupima uzito wa magari yanayoingia kupeleka taka na kuzimwaga.
Pia Kashaga alibainisha kutokuwepo kwa eneo la kutosha linalozungka dampo hilo ambalo lilipaswa kuwa na urefu wa mita 250 katika pande zote.