PANGA PANGUA DAWASA, WATEKELEZA AGIZO LA WAZIRI WAONGEZA MIKOA 7

 

 Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv


Uongozi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) umefanya mabadiliko ya watendaji katika nafasi mbalimbali pamoja na kuongeza mikoa ya kihuduma saba.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Mhandisi Cyprian Luhemeja amefanya mabadiliko hayo kufuatia agizo la Waziri wa Maji Jumaa Aweso hapo jana.

Waziri Aweso alitoa maagizo hayo ya kutaka mameneja wa mikoa ya kihuduma wabadilishwe ili ufanisi wa kazi uimarike na kuacha mazoea katika kazi.

Katika mabadiliko hayo,  mameneja wa mikoa ya kihuduma wamebadilishwa nafasi zao ambao ni Mhandisi Pascal Fumbuka -DAWASA Chalinze, Alpha Ambokile - DAWASA Kibaha, Judith Singinika - DAWASA Kawe, Gilbert Masawe -DAWASA Ubungo, Alex Ngwandu- DAWASA Kisarawe, Christian Kaoneka -DAWASA Bagamoyo
Erasto Emmanuel -DAWASA Kinondoni na Victoria Masele -DAWASA Tegeta.

Wengine ni  Mhandisi Boniface Philemon -DAWASA Tabata, Jullieth John -DAWASA Magomeni, Tumain Mhondwa - DAWASA Kigamboni,  Mhandisi Damson Mponjoli-DAWASA Ukonga, Abraham Mwanyamaki -DAWASA Mkuranga, Crossman Makele -DAWASA Temeke na Mhandisi Honest Makoi -DAWASA Ilala. 

Aidha, DAWASA imeongeza mikoa ya kihuduma 7 ili kuzidi kuwafikia wananchi zaidi ambapo tayari uongozi umefanya uteuzi wa mameneja wake ambao ni 
 Mhandisi Redemta James -DAWASA Mbagala, Mhadisi Deosdedith Kimaro- DAWASA Mivumoni, Mhandisi Edson Robert -DAWASA Makongo,  Haruna Taratibu -DAWASA Mabwepande, Mhandisi Mkashida Kavishe -DAWASA Mapinga, Burton Mwalupaso- DAWASA KInyerezi, Elizabeth Sankere -DAWASA Kibamba.

Pia, Afisa Mtendaji Mkuu amefanya mabadiliko katika menejimenti ikiwemo katkka nafasi ya Meneja Rasilimali watu ikichukuliwa Bernadetha Mwabusila  na Stella Fumbuka katika nafasi ya Meneja Utawala.

Post a Comment

Previous Post Next Post