Mhandisi John Chacha Nyamuhanga, mratibu ufundi katika mradi wa Regrow, akizungumza kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo katika kilimo cha umwagiliaji. |
Kaimu Mkurugenzi Mkuu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali akitoa wito kwa wakulima w akilimo cha umwagiliaji kuhusiana na tozo na utunzaji wa miundombinu ya kilimo hicho. |
NA MWANDISHI WETU - DODOMA
Wakulima wakilimo cha umwagiliaji nchini wamepewa wito wakuchangia tozo za umwagiliaji katika skimu za kilimo cha umwagiliaji katika ukanda wa nyanda za juu kusini ili kuweza kuimarisha miundombinu ya kilimo hicho kwakufanyia maboresho ya miundombinu hiyo inapotokea kuharibiwa na dharura kama mafuriko yatokanayo na mvua kubwa.
Hayo yamelezwa mapema leo mjini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagliaji Bw. Daudi Kaali ambapo akitolea mfano wa skimu za kilimo cha umwagiliaji zilizoko katika ukanda wa nyanda za juu kusini hususani katika mkoa Mbeya, ambako ni kati ya sehemu ambapo mradi wa REGROW unatekelezwa.
Bw.Kaali alisema kuwa,miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji itakapotunzwa vizuri na kuwaendelevu kutakuwa na ufanisi wa matumizi ya maji yatakayoleta matokeo makubwa katika upatikanaji wa maji katika mto Ruaha mkuu hasa wakati wa kiangazi.
Kwa upande wake Mhandisi John Chacha Nyamuhanga, Mratibu wa kiufundi wa mradi wa Regrow kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji alisema kuwa,kupitia mradi huo Tume ya taifa ya Umwagiliaji inajukumu la kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji kwa kujenga mabanio, mifereji mikuu na midogo,nakuhakikisha kuna ufanisi mkubwa wa matumizi ya maji katika shughuli za Umwagiliaji.
Akizungumzia kuwepo kwa mfuko wa Maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji, Afisa Mwandamizi kutoka katika Idara ya Uendeshaji na mafunzo Bw. Clavery Makoti, alisema kuwa,Sekta yakilimo cha umwagilaji ilikuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za uchakavu na uharibifu wa miondombinu ya umwagiliaji hivyo kupitia sheria ya umwagiliaji serikali ikaona kila sababu yakuanzisha mfuko huo ilikuweza kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta hivyo.
“Mfuko huo ulioanzishwa mwezi September mwaka huu mpaka sasa umewezakurekebisha skimu ya Ruaha Mbuyuni, na Pawaga na kiasi cha fedha shilingi milioni 410 zimetengwa kutumika kuboresha miondombinu ya Iringa na kilolo.” Alisema.
Awali, Mkurugenzi msaidizi idara ya uendeshaji kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw.Enterbert Nyoni alisema,idara yake inajukumu la uendeshaji wa mafunzo katika skimu za umwagiliaji ili skimu hizo ziweze kuimarika na kuleta tija ,idara huwafundisha wakulima mambo mbalimbali yakiwemo yanayohusu sheria ndogondogo za umwagiliaji matumizi sahihi ya fedha na matumizi bora ya maji kupitia kalenda.
Aliongeza kw akusema kuwa, mapokeo na muitikio wa mafunzo kwa wakulima ni chanya na kwani mpaka sasa wameshaanza kuona faida yakuwepo kwa mfuko wa maendeleo ya umwagiliaji.
Mradi huo wa Regrow unaotekelezwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na utalii kwa kushirikiana na taasisi zingine za serikali ikiwemo Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na bodi ya maji bonde la Rufiji, unalenga kuongeza utalii kusini mwa Tanzania na kukuza shughuli mbaadala za kiuchumi katika jamii zinazozunguka eneo unakotekelzwa Mradi katika hifadhi za Taifa za Ruaha, Mikumi,Udzungwa na MwalimuNyerere