TIA YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WASTAAFU WA WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.

 

Picha ya Pamoja ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo akiwa katika picha ya Pamoja wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati mafunzo yalitolewa na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA).


Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Profesa Carolyne Nombo akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Elimu ,Sayansi na Teknolojia Jonathan Kabengwe wakati wa kufungua mafunzo ya watumishi wa Wizara hiyo wanaotarajia kustaafu katika chuo Cha Ualimu Kigurunyembe mkoani Morogoro.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt.Leonard Akwilapo wakisaliimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Profesa Carolyne Nombo wakati ufunguzi wa mafunzo ya watumishi ya wizara hiyo wanatarajia kustaafu ambapo mafunzo hayo yanatolewa na TIA.

******************************

 *Katibu Mkuu Akwilapo afungua mafunzo ya watumishi wastaafu.

*Aahidi kupeleka mafao ya wafanyakazi kila mwezi PSSSF.

Na Mwandishi wetu, Morogoro

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema itahakikisha  michango ya watumishi  waliopo chini ya wizara hiyo inawasilishwa kwa wakati kwenye  Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ili  wanapofikia umri wa kustaafu wapate mafao  yanayostahiki  kwa wakati ambayo yatawawezesha kushiriki  shughuli za maendeleo ya kupitia miradi ya kiuchumi watakayoiazisha .

Katibu Mkuu  wizara hiyo, Dk Leonard Akwilapo ,alisema hayo leo ( Nov 23) katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Morogoro  mjini wakati akifungua  mafunzo maalumu ya watumishi  wanaotarajia kustaafu  yaliyokuwa yakitolewa na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA)wapatao 223  kutoka makao makuu ya wizara , Vyuo vya maendeleo ya wananchi , Vyuo vya Ualimu  na Idara ya uthibiti wa shule  ambao wapo  chini ya wizara hiyo .

Hivyo , aliwataka watumishi wanaotarajia kustaafu kupitia kumbukumbu zao  ili kubaini iwapo michango inawasilsihwa kwenye  mfuko wa hifadhi wa  PSSSF ili baadaye wasiweze kupata shida ya kulipwa mafao yao

“ Kwa sasa hivi tunahakikisha tunapitia kumbukumbu za kila mtumishi  ili kuona  mchango wa  kila mwezi inaenda  , huko nyuma kulikuwa na tatizo kidogo  palikuwepo na madeni ya ajabu ajabu , lakini  hivi sasa mambo  yamenyooka   ni kutokana na mfumo uliowekwa “ alisema Dk Akwilapo.

Dk Akwilapo, aliwaagiza watendaji wa wizara hiyo kuhakikisha wanapitia nyaraka zote za watumishi ili kuona   mapungufu yanayojitokeza  na kama kuna changamoto na ziweze kurekebishwa kabla ya kufikia juni mwaka 2021  kwa lengo la zielkebisha kasoro hizo.

Pia aliwataka watumishi  wa wizara hiyo kufuatilia taarifa zao  za malipo kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma  kwa ajili ya kupata uhakika wa michango yao iwapo inapelekwa na endapo kunamatatizo   utatuzi wake ufanyika  kabla ya kufikia muda wa kistaafu kwao utumishi wa umma.

Katibu mkuu , alisema lengo la  wizara ni  kiuona mafuzo kama hayo  yanatolewa kwa watumishi inabobakia miaka mitano ya  kustaafu kwao ili wapate  uzoefu  na kikifanyia kazi kile wanachojifunza  na  baada ya kustaafu  waweze kuendelea na uendeshaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi bila ya kuwa na wasiwasi.

 “ Nafikiri ni wakati mzuri wa kutolewa kwa mafunzo haya  mtumishi akibakiwa na  miaka mitano ya kustaafu  ili kuwajengewa uwezo  kuwa na mpango endelevu wa namna ya uendeshaji wa miradi mbalimbali ya kibiashara na kilimo “ alisema Dk Akwilapo.

Kwa upande wake Afisa  Mtendaji Mkuu  wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania(TIA), Profesa  Carolyne Nombo, katika hotuba yake  ,alisema  kustaafu huambatana na changamoto mbalimbai zikiwemo za kiuchumi , kifanya na kisakolojia hasa pale mstaafu anapoona majumkumu na uhitaji wake katyika jamii unapungua.

“ Ajira inapofikia tamati huathiri moja  kwa moja  ratiba nzima ya maisha ya mstaafu  kwa mgano muda gani aamke, muda gani wa kula , muda gani wa kupumzika nyumbani na mengineyo” alisema Profesa  Nombo.

Profesa  Nombo, alisema jambo la msingi analoweza kufanya mfanyakazi ni kufanya maandalizi mapema kabla ya kustaafu ili kukabiliana na changamoto zitakazojidhirisha mbeleni  na moja walo ni kujenga tabia ya kujiwekea akina  , kutafuta vyanzo mbadala vya mapato   na kujali afya .

“ Mstaafu unakatiwa kuwa makoni na mwangalifu ikiwezekana anza kukwepa kuchukua madeni mapya , ishi maisha ya kawaida nay a staha” alisema Ofisa  Mtendaji Mkuu  wa TIA.

Naye Mshauri Mwelekezi na Mratibu wa Mafunzo wa TIA , Dk Hasanal Isaya  , alisema mafunzo hayo ya wastaafu yamejumishia mada mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyngine zitawasidia wastaafu katika utelelezaji wa majukumu yao ya maisha baada ya kustaafu , ili kufikia malengo na ndoto zao za maisha   baada ya ajira .

Dk  Isaya, alitaja baadhi ya mada hizo ni  pamoja na faida ya kujindaa kabla ya kustaafu, kutengeneza mipango ya biashara  , matumizi ya kiinua mgogo na mikopo , kuendeleza  na kukuza mtaji katika  biashara , sababu za kuwekeza katika biashara ,sifa za mjasiliamali , mafanikio katika biashara , utunzaji wa kumbukumbu  na taarifa za fedha ,  na faida ya lishe bora na mazoezi kwa wastaafu.

Nao washiriki wa mafunzo hayo kupitia  Mwenyekiti wao ambaye ni  Mthibiti Ubora wa Shule , Frenk Timotheo , alimwomba Katibu mkuu wa wizara hiyo kuangalia namna kuwaingizia  madaraja yao ambayo  hayajafanyiwa kazi  ili wanapostaafu waweze kupata mafao yao naayostahiki na madaraja yao .

Pia alimwomba Katibu mkuu  kutoa kipaumbele  wanapowasilisha barua za kustaafu ikiwa na malipo yao kufanyika kwa haraka ili kuwaepusha   kukopa fedha  sehemu mbazo zi salama kwa ajili ya kuendesha maisha yao  wakisuburi kulipwa mafao ya kustaafu jambo  linaweza kuleta athari kwao.

Post a Comment

Previous Post Next Post