BENKI YA CRDB YAZINDUA KAMPENI YA “TUPO MTAANI KWAKO”

 

Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akiwa kwenye gari la CRDB Wakala kuashiria uzindua rasmi wa kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako” ambayo inalenga kuhamasisha matumizi ya huduma za benki pamoja na kuwaunganisha Watanzania walio wengi kutumia huduma za Benki yao ya CRDB. Kushoto ni Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya CRDB, Badru Idd.
Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akizungumza na waandhishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako” ambayo inalenga kuhamasisha matumizi ya huduma za benki pamoja na kuwaunganisha Watanzania walio wengi kutumia huduma za Benki yao ya CRDB. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif.
Benki ya CRDB imezindua kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako” ambayo inalenga katika kuhamasisha matumiziya huduma za benki pamoja na kuwaunganisha Watanzania walio wengi kutumia huduma za Benki yao ya CRDB.

Akizungumza katika uzinduzi huo ambao ulifanyika katika makao makuu ya Benki ya CRDB na kuhudhuriwa na wateja na CRDB Wakala, Afisa Biashara Mkuu wa benki hiyo, Dkt. Joseph Witts alisema kampeni hiyo ya “Tupo Mtaani Kwako” itasaidia kuelimisha wateja juu ya fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB, kutoa elimu na ushauri wa masuala ya fedha, pamoja na kuwaunganisha wateja na huduma zinazotolewa na benki hiyo ikiwamo kufungua akaunti

Post a Comment

Previous Post Next Post