TFS WAKUMBUKA MCHANGO WA HAYATI MWALIMU NYERERE KATIKA UHIFADHI WA MISITU .

 

*********************************

Akizungumza katika siku ya kumbukizi ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Shaban Kiula ambaye ni Afisa Misitu Mkuu TFS kanda ya Mashariki tarehe 14 /10/2020 katika Hifadhi ya Msitu wa Mazingira asilia Pugu amesema kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa kielelezo bora cha Uhifadhi wa Misitu.

“Mwalimu Nyerere alisema  Deni la kukata miti bila kupanda ni Deni haramu.unawaibia ambao hawajazaliwa.kwa hiyo yeye alijua umuhimu wa kuhifadhi hii misitu na yeye atabaki kuwa kielelezo bora cha Uhifadhi kutokana na mchango wake Kiula.

Nao Wadau wa Misitu na Utalii kupitia vipindi vya Wanawake kutoka Jiji la Dar es salaam kikiwemo kikundi cha CODECO,Wanawake na Mafanikio na Wanawake Wazalendo kwanza, wameeleza jinsi wanavyofurahia uwepo wa Hifadhi za Misitu Asilia ambayo imekuwa fursa muhimu ya watu kufanya utalii wa ndani.

“Tunashukuru TFS kwa kuandaa hii siku ya kumbukizi ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere , tumemuenzi kwenye kitu alichokipenda sana, alipenda Misitu iwepo ndiyo maana tumeweza kuja kutalii. Hii ni Fursa ya kila mtanzania kufanya Utalii wa ndani “Veradiana Nsongo, Mratibu Msaidizi CODECO.

Naye Maria Mapunda ambaye ni kiongozi wa Kikundi cha Wanawake na Mafanikio ameshukuru TFS kwa kuipa thamani siku ya kumbukizi ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na kuandaa utaratibu wa kufanya utalii katika Vivutio mbalimbali vya Utalii vinavyopatikana katika Hifadhi ya Msitu wa Mazingira asilia Pugu.

Post a Comment

Previous Post Next Post