*********************************************
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bw.Edwin Rutageruka akifungua kikao cha Wadau wa Kliniki ya Biashara kutoka Taasisi Binafsi na Taasisi za Umma ambazo miongoni mwa Taasisi hizo ni EPZA, BRELA, TIC, GS1, TRA, WMA, NBC, NEEC, TBS, SIDO, FFC, CBE, na TFS. Lengo la kikao ni kufanya tathimini na kujadili mikakati ya maboresho ya utoaji huduma ya Kliniki ya Biashara.
Kliniki ya Biashara husimamiwa na TanTrade na kudhaminiwa na Benki ya NBC ambapo huwakutanisha wataalam wa Biashara kutoka Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi ambao hushirikiana katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Wafanyabiashara hapa nchi.
Itakumbukwa kuwa tarehe 14 Oktoba, 2020 Tanzania kupitia huduma ya Kliniki ya Biashara inayosimamiwa na TanTrade ilitajwa kuwa mshindi wa tatu wa dunia(Best use of partnership category) na wa pekee kutoka nchi za Afrika kwenye Tuzo za Taasisi zinazosimamia Biashara duniani (WTPO Awards 2020)