DKT.ZAINABU CHAULA AZINDUA MINARA YA MAWASILIANO WILAYANI CHATO

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula (wa kwanza kulia), akikata utepe kuzindua mnara wa mawasiliano wa Igando mkoani Geita. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhandisi Charles Kabeho na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Waziri Kindamba

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula akimsikiliza kwa makini Meneja Mipango Mtandao wa Shirika la Mawasiliano Tanzania, Mhandisi Innocent Msasi akitoa maelezo kuhusu mnara wa mawasiliano wa Naybilezi, Geita baada ya kuzinduliwa rasmi na katibu Mkuu huyo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Chato, Denis Bandisa baada ya kuzindua mnara wa mawasiliano wa Igando mkoani humo. Anayesikiliza kulia ni Mkuu wam Wilaya ya Chato, Mhandisi Charles Kabeho

Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Charles Kabeho, akizungumza na wananchi wa Igando kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula (aliyevaa kilemba), kuzindua mnara wa mawasiliano ya simu kijijini humo mkoani Geita

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula (aliyevaa kilemba) kuhusu gharama za ujenzi wa mnara wa mawasiliano wa Nyabilezi na Igando kabla ya uzinduzi wa minara hiyo kijijini Igando mkoani Geita

Wananchi wa Kijiji cha Igando kilichopo mkoani Geita wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula (hayupo pichani) akizungumza nao baada ya kuzindua mnara wa mawasiliano kijijini humo. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Charles Kabeho

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula akimpatia Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Charles Kabeho, vitabu vyenye orodha ya maeneo ilikojengwa minara ya mawasiliano kwa kutumia ruzuku ya Serikali iliyotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote nchi nzima

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt. Zainabu Chaula (aliyevaa kilemba), akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Charles Kabeho (aliyesimama kulia) na wananchi wa Kijiji cha Igando baada ya Katibu Mkuu huyo kuzindua mnara wa mawasiliano kiijijini humo.

…………………………………………………………….

*Asema Mawasiliano ni uchumi, maendeleo, uwekezaji na huduma 

*Atoa rai kwa wananchi kutumia mawasiliano kudumisha amani na mshikamano

Na Prisca Ulomi, WUUM, Chato

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Dkt.Zainabu Chaula amezindua minara miwili ya mawasiliano iliyopo kwenye kijiiji cha Nyabilezi na Igando vilivyopo wilayani Chato mkoani Geita ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za mawasiliano

Dkt. Chaula amesema kuwa ujenzi wa minara hiyo umefanyika kwenye vijiji hivyo baada ya wananchi kuomba huduma za mawasiliano na Serikali kujiridhisha kuwa mawasiliano hayapo kwenye maeneo hayo na kuamua kujenga minara hiyo kwa kutumia ruzuku ya Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambapo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi milioni mia tano

Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za mawasiliano kwa kuwa mawasiliano ni uchumi na Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa kujenga Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ambao ni sawa na barabara kuu kwa ajili ya kupitisha ya uhakika na kwa wakati ambapo minara hiyo imeunganishwa kwenye Mkongo huo ili kuweza kuwapatia wananchi huduma

Naye Katibu Tawala wa Mkoamwa Geita, Denis Bandesi amesema kuwa miundombinu ya mawasiliano ambayo imewekwa kwenye maeneo hayo itawasaidia wananchi kufanya mawasiliano na kuendesha biashara zao ili kuhakikisha kuwa uchumi wa kati unamgusa mwananchi pale alipo kwa maana uzalishaji atakaokuwa ameufanya atakuwa na uhakika  wapi apeleke biashara yake kwa maana ya uhakika wa bei nzuri mahali soko lililopo

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba amewataka wananchi kuchangamkia fursa ya kuwa mawakala wa huduma za mawasiliano wa Shirika hilo kwa kuwa TTCL inatoa kamisheni mara mbili ya kampuni nyingine za mawasiliano na fedha inayopatikana inarudi Serikalini na ameomba wananchi wailinde miundombinu hiyo kwa kuwa imetumia fedha za Serikali kujengwa na ikiharibika wananchi watakosa mawasiliano

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhandisi Charles Kabeho ameahidi kuwa atahakikisha miundombinu hiyo inalindwa ili wananchi wanufaike na huduma za mawasiliano kwa kuwa hapo awali hapakuwa na huduma za mawasiliano ila kwa sasa mtandao wa TTCL uko vizuri na wananchi wanaweza kupiga simu ndani na nje ya Tanzania

Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba amesema kuwa UCSAF ina jukumu la kupeleka mawasiliano vijijini ambapo mpaka sasa UCSAF ina miradi ya ujenzi wa minara ya mawasiliano sehemu mbali mbali nchini kwenye kata 998 ambapo hadi sasa ujenzi umekamilika kwenye kata 903 ambapo zaidi ya wananchi wapatao milioni tano wanapata huduma za mawasilian

Post a Comment

Previous Post Next Post