VIJIJI VYOTE KUPATIA UMEME KUPITIA MRADI WA UJAZILIZI

 

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Maza , kata ya Mazae, Wilaya ya Mpwapwa,Mkoani Dodoma, wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa usambazaji umeme vijijini

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akifurahi mara baada ya kukata utepe kuashiri kuwashwa kwa umeme katika Kijiji cha Mazae kilichopo katika kata ya Mazae, Wilaya ya Mpwapwa,Mkoani Dodoma

 

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu(mwenye kilemba) akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Morogoro wakiwa katika ziara ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme katika maeneo mbalimbali ya  Kijiji cha Lumuma,kata ya Lumuma, Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro.

…………………………………………………………..
Na Farida Said, Morogoro.
Katika kuhakikisha vijiji vyote vinapata umeme hapa Nchini Naibu Waziri wa Nishati Mhe Subira Mgalu amelitaka shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Morogoro kusimamia kikamilifu Mradi wa ujazilizi katika Kijiji cha Lumuma Wilayani Kilosa Mkoani humo.
Akiwa katika Kijiji Cha Lumuma kwenye hafla ya kuwasha na kizindua Mradi wa Umeme uliojengwa na TANESCO Mkoa wa Morogoro Naibu Waziri Mgalu amesema Serikali ya awamu ya tano inayongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli imefanya kazi kubwa ya kuhakikisha kila Kijiji hapa Nchini kinafikiwa na Nishti ya Umeme,ili wananchi wake waweze kutumia nishati hiyo katika kukuza uchumi.
Aidha, amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupeleka Mradi wa ujazilizi katika Kijiji hicho ili wananchi wote wa kijiji hicho waweze kufikiwa na Nishati hiyo ,huku akisisitiza usimamizi mzuri kwa mkandarasi atakayepewa kazi ya kujenga Mradi huo
Katika hatua nyingine amesema upatikanaji wa Nishati ya Umeme katika Kijiji hicho kutainua uchumi wa Wilaya ya Kilosa, kwani kupitia Nishati hiyo kutawasaidia wananchi kuanzisha Viwanda vikubwa na vidogo vitakavyo saidia kukuza uchumi wa Kijiji na Wilaya kwa ujumla.
Aidha Mradi wa upelekaji umeme katika kijiji cha Lumuma ni kati ya Miradi inayotekelezwa na TANESCO Mkoa wa Morogoro kufuatia maelekezo ya Naibu Waziri wa Nishati Mhe Subila Mgalu aliyoyatoa Mwezi 9,2019 alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kukagua maeneo ambayo hayana huduma ya umeme Wilayani Kilosa.
Hata hivyo, mradi huo umegharimu jumla ya 99,204,240.97 Fedha za Kitanzania, huku zaidi ya Wanajiji 238 wameunganishwa na huduma ya umeme kupitia Mradi huo,ambapo utawanufaisha katika matumizi mbalimbali ikiwemo katika Viwanda,Kilimo na Biashara mbalimbali.

Post a Comment

Previous Post Next Post