TANZANIA NA DENMARK ZAIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA YA MAJI

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Mette Dissing Spandet katika kikao kilichohusu ushirikiano baina ya nchi hizo kwenye Sekta ya Maji.

Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Mette Dissing Spandet (mwisho kulia) akiwa na wajumbe alioongozana nao Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Denmark, Mette Bech (katikati) na Msimamizi wa Idara ya Uwekezaji na Biashara katika Ubalozi wa Denmark, Oscar Mkude

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga (kulia) akiwa na Mkurugenzi Msaidizi Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini, Pamella Temu.

Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Mette Dissing Spandet (kulia) pamoja na Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Denmark, Mette Bech

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akiwa pamoja na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Mette Dissing Spandet mara baada ya kikao kilichohusu ushirikiano baina ya nchi hizo kwenye Sekta ya Maji.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Mette Dissing Spandet wakiwa pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Maji na Ubalozi wa Denmark baada ya kikao kilichohusu ushirikiano baina ya nchi hizo kwenye Sekta ya Maji.

………………………………………………………………….

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amekutana na kuzungumza Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Mette Dissing Spandet kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo kwenye Sekta ya Maji.

Mazungumzo hayo ya awali yalilenga ufadhili wa utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji hususan kwenye maeneo ya usambazaji wa majisafi na usafi wa mazingira kwenye  majiji ya Dodoma na Dar es Salaam, kabla ya kukutana tena na kujadili masuala ya kiufundi katika kutekeleza miradi hiyo.

Kikao hicho kilihusisha wajumbe kutoka Wizara ya Maji, Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Denmark, Mette Bech pamoja na Msimamizi wa Idara ya Uwekezaji na Biashara katika Ubalozi wa Denmark, Oscar Mkude.

Post a Comment

Previous Post Next Post