NAIBU WAZIRI AWESO AIPONGEZA TMA, ATAKA IENDELEE KUWASAIDIA WAKULIMA

Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso (wa tatu kushoto) akisisitiza jambo alipotembelea Banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanayoendelea mkoani Morogoro. Kushoto ni Mtaalam wa Hali ya Hewa kutoka TMA, Dk. Alfred Kandowe akimsikiliza kwa makini, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Godwin Gondwe alieambatana na Naibu Waziri. 

 

Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso akizungumza ndani ya Banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanayoendelea mkoani Morogoro. Kushoto ni Mtaalam wa Hali ya Hewa kutoka TMA, Dk. Alfred Kandowe akimsikiliza kwa makini. 

 

Mtaalam wa Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk. Alfred Kandowe (mwenye fulana nyeupe) akimwelezea Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso (wa pili kulia) alipotembelea Banda la TM kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanayoendelea mkoani Morogoro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Godwin Gondwe. 

 

Mtaalam wa Hali ya Hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk. Alfred Kandowe akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso alipotembelea Banda la TM kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanayoendelea mkoani Morogoro.

 

Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso akisaini kitabu cha wageni ndani ya Banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki  alipotembelea Banda hilo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Godwin Gondwe. 
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
 
NAIBU Waziri wa Maji, Juma Aweso ameipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kwa juhudi wanazozifanya kuwasaidia wakulima kupitia taarifa zao za hali ya hewa na kuwataka kuhakikisha taarifa hizo zinaendelea kuwa ufumbuzi wa changamoto za wakulima.
Naibu Waziri,  Aweso ameyasema hayo alipotembelea Banda la  TMA kujionea shughuli zao kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki yanayoendelea mkoani Morogoro.
“…Naomba mhakikishe taarifa zenu nisahihi na zinaendelea kumsaidia mkulimakwenye shughuli zake za kilimo…mjikite na kuona hii ni kazi inayotakiwa kutolewa kwa umakini ili iwe na msaada, msikimbilie kutoa tu bila kujiridhisha,” alisisitiza Naibu Waziri,  Aweso akizungumza ndani ya banda hilo.
Pia aliitaka TMA kuhakikisha taarifa wanazozitoa zisizue hofu kwa wananchi bali kuwa msaada kwenye shughuli zao, kwani wananchi wanamatumaini makubwa na taasisi hiyo kuwasaidia katika suala ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Kwa upande wake, Mtaalam wa Hali ya Hewa kutoka TMA, Dk. Alfred Kandowe alimwelezea Naibu Waziri Aweso kuwa kwa sasa TMA ina mfumo maalumu wa utoaji taarifa za hali ya hewa kwa wananchi wenye simu za kawaida kabisa (zisizo simu janja) kupitia meseji za kawaida ujulikanao kama ‘farm sms’ ambao usambaza taarifa kwa wakati kwa wakulima, wafugaji na wavuvi waliojiunga ambao umekuwa na msaada kwao.
“Ili mteja wetu yeyote aweze kujiunga kwenye mfumo huu wa kupata taarifa za hali ya hewa kupitia simu za kiganjani, kuna fomu zetu ambazo kila tunapopita huwa tunawapa wateja na hata wadau wetu wanajaza taarifa zao…na taarifa ya msingi ni namba ya simu ya mteja ambayo itapokea meseji, anataka kupata taarifa kwenye eneo gani na akitaja tunamtengenezea eneo husika na kumtumia..,”
Aidha aliongeza kuwa utoaji wa taarifa za hali ya hewa umeboreshwa zaidi hivyo mteja anaweza kupata taarifa hizo kwa eneo lake tu na hata kwa muda fulani, kulingana na mahitaji ya mteja wetu. “…Mkulima, mfugaji au mvuvi yeyote akitaka taarifa kwa eneo lake tu tunaweza kumtumia kulingana na mahitaji yake, na atazipokea moja kwa moja kwenye namba ya simu aliyotupatia,” alisema Ofisa huyo

Post a Comment

Previous Post Next Post