KUSAYA AIPONGEZA TaCRI/COFFEE AFRICA KWA KUZALISHA MICHE BORA ELFU 70

 

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akipata maelezo kuhusu uzalishaji wa miche bora ya kahawa aina ya robusta na arabika elfu 70 kutoka kwa Aretas Urassa, Afisa Ugani na Mafunzo kutoka Kituo cha uzalishaji wa miche bora ya kahawa cha TaCRI Maruku katika Halmashauri ya Bukoba Vijijni, wakati wa ziara yake mkoani Kagera

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akiangalia mche bora wa kahawa aina ya arabika wakati wa ziara yake ya kutembelea shughuli za Sekta ya Kilimo katika Kituo cha uzalishaji wa miche bora ya kahawa cha TaCRI Maruku katika Halmashauri ya Bukoba Vijijni, mkoani Kagera

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akipata maelezo kuhusu ubora wa madaraja ya kahawa kutoka kwa Dkt. Nyabisi Maliyatabu, Meneja wa Kanda ya TaCRI Maruku katika Halmashauri ya Bukoba Vijijni, wakati wa ziara yake mkoani Kagera

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya akiangalia mti wa kahawa aina ya robusta katika shamba la mafunzo la Wanachuo wa Chuo cha Kilimo Maruku (MATI Maruku) katika Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Vijijni, wakati wa ziara yake mkoani Kagera

 ………………………………………………………………………….

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya ameipongeza Taasisi ya Utafiti wa Miche Bora ya  Kahawa (TaCRI) pamoja na Mradi wa Coffee Africa kwa kuzalisha zaidi ya miche bora ya kahawa aina ya robusta, miche elfu sabini (70,000) katika kipindi cha miezi mitano, kuanzia mwezi Machi hadi Agosti, 2020.

Katibu Mkuu Kusaya alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea kitalu maalum cha uzalishaji wa miche bora ya kahawa wakati wa ziara yake ya kutembelea Kituo cha TaCRI Maruku, katika Halmashauri ya wilaya ya Bukoba Mjini, leo tarehe 10 Agosti, 2020 wakati wa ziara yake ya kutembelea na kukagua shughuli za maendeleo ya Sekta ya Kilimo mkoani Kagera.

Katibu Mkuu Kusaya amesema tija na kuongezeka kwa uzalishaji wa zao la kahawa kutoka tani elfu 50 unategemea kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa miche bora yenye ukinzani dhidi ya ugonjwa hatari wa chulebuni pamoja na kutu ya kahawa.

“Nawapongeza TaCRI pamoja na Mradi wa Coffee Africa kwa kuzalisha miche bora elfu 70 katika kipindi cha miezi mitano tu, niwapongeze pia kwa kutoa miche hii bure kwa Wakulima wetu”. Amekaririwa Katibu Mkuu Kusaya.

Post a Comment

Previous Post Next Post